Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo wa CCM wasakwa kwa ulawiti, ubakaji
Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wa CCM wasakwa kwa ulawiti, ubakaji

Pingu
Spread the love

KATIBU Mwenezi wa CCM Kata ya Mkolani, Zephilin Michael na Katibu Mwenezi wa chama hicho katika kata ya Buhongwa, Hassan Bushangama wanasakwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za ubakaji na ulawiti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza liyotolewa leo tarehe 31 Oktoba 2018 na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna inaeleza kuwa, Mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni Michael anadaiwa kutenda kosa la ulawiti dhidi ya kijana wake wa kazi tarehe 26 Oktoba 2018.

Michael anadaiwa kumpangishia kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 chumba katika nyumba ya wageni iliyopo katika Kata ya Mkolani, eneo ambalo alilotumia kumfanyia ukatili huo, kisha kutoroka baada ya kijana kupiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa raia wema.

Taarifa hiyo ianeleza kuwa, mtuhumiwa wa pili ambaye ni Bushangama anadaiwa kumbaka na kumpatia ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17, wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Buhongwa.

Bushangama anasakwa na Jeshi la Polisi baada ya kutoroka wakati polisi wakiendelea na taratibu za kumfikisha mahakamani.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili,Jafari Swalehe na Mgassa Carlos wanaodaiwa kumtorosha mtuhumiwa huyo, ambao awali walikuwa ni wadhamini wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!