Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo wa CCM Mwanza ‘wavuana nguo’
Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wa CCM Mwanza ‘wavuana nguo’

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire. Picha ndogo, Kiomoni Kibamba, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Spread the love

MSUGUANO wa Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire (CCM) na Mkurugenzi wa jiji hilo, Kiomoni Kibamba, limefikia katika hatua mbaya baada ya wawili hao kutuhumiana hadharani, kila mmoja akimtupia madongo mwenzake, anaandika Moses Mseti.

Siku moja baada ya Meya Bwire kumtuhumu, Mkurugenzi Kibamba kuratibu mbinu chafu za madiwani kumpigia kura za kutokuwa na imani naye, mkurugenzi huyo ameibuka na kuanika uchafu wa meya huyo.

Mkurugenzi Kibamba baada ya kushushiwa tuhuma hizo, MwanaHALISI Online ilimtafuta mkurugenzi huyo ofisini kwake ili kuzungumzia suala hilo, ambapo Kibamba alifunguka kusema kuwa Meya Bwire amekuwa akimshinikiza ampe fedha kinyume na utaratibu kwa maslahi yake binafsi.

Kibamba amesema hivi karibuni meya huyo alimuita ofisini kwake na kumtaka akamuombee Sh. 2 milioni kutoka kwa mkandarasi anayejenga dampo la kisasa lililopo kata ya Buhongwa lakini aligoma kufanya hivyo.

Mkurugenzi huyo amedai kwamba meya alimshinikiza na kumtaka aache kufuatilia mgogoro wa viwanja (vilivyopo Mahina) ambavyo kwa sasa vimeporwa na Bwire licha ya jiji kuwalipa fidia wananchi wa maeneo hayo tangu mwaka 2013.

Kibamba pia amesema katika viwanja ambavyo meya huyo anagoma kuvirudishwa kwa halmashauri hiyo, alivipata kwa njia ya kughushi nyaraka na kwamba tayari wamefikisha suala hilo polisi ambayo inaendelea na uchunguzi.

“Yeye meya huwa ana mambo yake, mambo yake ndiyo anayoyafanya kuwa msimamo wa madiwani, Aprili 6, mwaka huu aliniita ofisini kwake na kunitaka nikamuombe rushwa ya milioni mbili kwa hao wakandarasi nikakataa.

“Huo ndiyo mwanzo wa hasira zake za kuanza kurusha shutuma dhidi yangu. Aligombea jiji kuchuma fedha na hapa hapachumiki, atapata haki yake ya kisheria. Anayosema kwamba kampuni zinazojenga mradi huo ni zangu sio kweli (huku akionyesha nakala ya wamiliki wa kampuni zinazojenga mradi huo),” amesema Kibamba na kuongeza.

“Katika watu waongo duniani mmoja wao ni Meya (James Bwire), kwanza na huo mradi wa maji anaosema upo chini ya kiwango ni wa mwaka 2009 na mimi sikuwepo Mwanza na niliukuta mradi umesimama kwa mwaka mmoja na nusu na madiwani hawajui waanzie wapi na mimi ndiyo nikaanza juhudi za kuhakikisha unafanya kazi na sasa unafanya kazi.”

Kibamba amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake, zinasababishwa na yeye kugoma kutoa fedha, pia alidai kwamba kuendelea kufanya hivyo kwa meya kutasababisha jiji la Mwanza kukosa fedha za miradi ya maendeleo zikiwemo zinazotarajiwa kutolewa na Benki ya Dunia kiasi cha Sh. 19 bilioni.

Kibamba amesema Aprili 21, 2017, baada ya meya kuanza maneno hayo madiwani walifanya ziara katika mradi wa dampo la kisasa (Buhongwa) ambapo kamati ya huduma ya jamii ilikwenda mara moja kwenye mradi.

Pia amesema kuwa tarehe hiyo hiyo meya aliwataka madiwani wenzake wagomee mradi huo lakini waligoma kufanya hivyo kwa kuwa marekebisho waliyokuwa wameagiza yafanyiwe kazi yalitekelezwa.

Kibamba amesema kuwa meya ndiye adui mkubwa wa maendeleo ya wananchi wa jiji la Mwanza kwa maslahi yake binafsi, kwa kuwa amekuwa kizungumza maneno bila kuwa na ushahidi wowote ule.

MwanaHALISI Online ilipomtafuta Meya Bwire kwa njia ya simu kuzungumzia madai alisema; “Hivi wewe Mseti (mwandishi) una tatizo gani na mimi.” Alihoji Meya na kukata simu.

Hata hivyo, alipotafufwa kwa mara ya pili simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno saa 6:50 mchana leo ukuelezea tuhuma hizo, haukujibiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!