Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Vigogo MSD wadaiwa kukwapua bil 1.6
Habari Mchanganyiko

Vigogo MSD wadaiwa kukwapua bil 1.6

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
Spread the love

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)  nchini Tanzania, Laurean Bwanakunu na mwenzake wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kushtakiwa kwa makosa matano yakiwemo kuitia mamlalaka hasara na  utakatishaji fedha kiasi cha Sh.1.6 bilioni. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Mwenzake ni Byekwaso Tabura ambaye ni kaimu mkurugenzi wa Lojistiki wa (MSD).

Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020 na Wakili wa Serikali Faraja Nguka akishirikiana na Fatma Waziri na Sophia Nyanda, mawakili wa Taasisi ya Kuzuiya na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mbele ya Hakimu Mkazi Mkui Rechard Kabate.

Shtaka la kwanza ni la kujihusisha na genge la uhalifu ambalo ni kinyume cha sheria linawakabiliwa watuhumiwa wote.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya tarehe 1 Julai 2016 na tarehe 30 Juni 2019 kwenye maeneo tofauti jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujipatia fedha.

Shtaka la pili ni kuisababishia mamlaka hasara ambapo watuhumiwa wote  wanakabiliwa na kosa hilo.

Inadaiwa kati ya tarehe 1 Julai 2016 na tarehe 30 Juni 2019 maeno ya Keko jijini Dar es Salaam kwa pamoja watuhumiwa  hao waliisababishia MSD kupata hasara ya Sh. 3.8 bilioni.

Shtaka la tatu, matumizi mabaya ya madaraka na kwamba shtaka hili linamkabili Bwanakunu, ambapo inadawa  kati ya tarehe 1 Julai 2016 na tarehe 30 Juni 2019 maeno ya Keko jijini Dar es Salaam, kwa makusudi  ametumia vibaya madaraka yake kwa kuwalipa wafanyakazi wa MSD Sh.3.8 bilioni kama nyongeza ya mishara na posho bila kuidhinishwa na Katibu Mkuu wa Utumishi.

Shtaka la nne, linawakabili watuhumiwa wote wawili ambalo ni kuisababishia mamlaka hasara.

Inadawa  kati ya tarehe 1 Julai 2016 na tarehe 30 Juni 2019 maeno ya Keko  jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini Tanzania, walihifadhi vibaya dawa na kusababisha zisiweze kutumika kitendo hicho kimeisababishia mamlaka hasara ya Sh. 85 milioni.

Shtaka la mwisho ni utakatishaji fedha, linawakabili watuhumiwa wote ambapo inadawa  kati ya tarehe 1 Julai 2016 na tarehe 30 Juni 2019 maeno ya Keko jijini Dar es Salaam kwa pamoja walijipatia Sh.1.6 bilioni wakijua zao la  matendo ya uhalifu.

Upelelezi wa shauri hilo haujakilimika. Hakimu Kabate amesema watuhumiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Juni 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!