SERIKALI ya Tanzania imewapandisha kizimbani aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk. John Pima na wenzake wanne kwa mashitaka kutenda makosa nane katika kesi za uhujumu uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani leo Ijumaa tarehe 17, Juni, 2022 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Pamoja na Dk. Pima washitakiwa wengine walipandishwa kizimbani ni waliokuwa wachumi wa jiji, Innocent Maduhu, Nuru Ginana na Alex Daniel na Mwwekahazina wa Jiji, Mariam Mshana ambaye hakuwepo mahakamani hapo.
Hata hivyo upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama kutoa hai ya wito na kukamatwa kwa mshatakiwa huyo ambaye ni wapili katika kesi zote.
Wakisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Bittony Mwakizu, katika kesi ya kwanza Dk. Pima, Mariam, Maduhu na Ginana wanakabiliwa na mashitaka manne ikiwemo ufujaji na ubadhirifu, matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai Mosi, 2022 ambapo washitakiwa watasomewa maelezo ya awali.
Itakumbukwa Mei 24 mwaka huu Waziri Mkuu KAssim Majaliwa aliwasimamisha kazi vigogo hao kwa tuhuma za ubadhirifu na kuagiza uchunguzi ufanyike na endapo watabainika kutenda makosa hao wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Leave a comment