Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo hawa kutikisa Kisutu leo
Habari za SiasaTangulizi

Vigogo hawa kutikisa Kisutu leo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na viongozi wengine wakiwasili mahakamani
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo inatarajia kusikiliza kesi ya vigogo tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti¬† Faki Sosi … (endelea).

Miongoni mwa vigogo hao ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa; Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Viongozi hao wa Chadema wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya mikisanyiko isiyoruhusiwa, kuhamasisha chuki, kushawishi watu kutoridhika na hata kula njama.

Viongozi hoa wanatarajiwa kuendelea na utaratibu wa kimahakama kwa kila mmoja kukabiliana na mashitaka yake.

Kumekuwepo na mahudhurio makubwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwenye kesi ya kisiasa inayomuhusisha Mbowe na Matiko.

Mbowe na Matiko walifikishwa mahakamani tarehe 23 Novemba 2018 kwa madai ya makosa kadhaa ikiwemo kufanya mkusanyiko usioruhusiwa na baadaye kukataliwa dhamana.

Kesi zingine zinazotarajiwa kusikilizwa leo ni pamoja na ya wafanyabiashara Seth Harbinder na James Rugemarila pia waliokuwa viongozi wa Timu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey na Nyange.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!