Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo Chadema kubanwa na kina Mdee mahakamani leo
Habari za Siasa

Vigogo Chadema kubanwa na kina Mdee mahakamani leo

Spread the love

 

WAJUMBE wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Azavel Lwaitama na Ruth Mollel, wanaanza kuhojiwa na mawakili wa wabunge viti maalum 19, katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu , jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni katika kesi Na. 36/2022 iliyofunguliwa na wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee, kupinga uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama kwa madai kuwa haikuwa halali, ambapo wanaiomba mahakama hiyo ifanye mapitio dhidi ya mchakato uliotumika katika suala hilo.

Leo tarehe 9 Machi 2023, Dk. Lwaitama na Mollel, wataanza kuhojiwa na mawakili wa kina Mdee, wakiongozwa na Wakili Ipilinga Panya, mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.

Vigogo hao wa Chadema, wanatarajiwa kuhojiwa kuhusu hati zao kinzani, walizowasilisha mahakamani hapo kujibu malalamiko ya wabunge hao kwamba walifukuzwa Chadema kinyume cha Sheria.

Hatua hiyo inajiri baada ya Jaji Mkeha, Jumatatu iliyopita kuwapa ruhusa wabunge hao kuwahoji maswali ya dodoso wajumbe sita wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema, ambapo mbali na Dk. Lwaitama na Mollel, wapo Mary Joackim, Francis Mushi, Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Hamis.

Mawakili wa Mdee na wenzake, waliomba kuwahoji vigogo hao baada ya mawakili wa Chadema, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, kuwahoji maswali ya dodoso wabunge watano kati ya nane waliyopanga kuwauliza kuhusu malalamiko yao ya kufukuzwa na chama hicho.

Miongoni mwa wabunge waliohojiwa ni, Nusrat Hanje, Hawa Mwaifunga, Grace Tendega na Jesca Kishoa.

Chadema kupitia mawakili wao, waliiomba mahakama hiyo iache kuwahoji wabunge wengine watatu, Mdee, Ester Bulaya na Esther Matiko, kwa madai kuwa wametosheka na majibu yaliyotolewa na wenzao.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online kwa taarifa zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!