Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari Vigogo ACT mbaroni kwa uchochezi, kukashifu viongozi wa Serikali
HabariSiasa

Vigogo ACT mbaroni kwa uchochezi, kukashifu viongozi wa Serikali

Spread the love

JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini limewakamata na kuwahoji watu wawili ambao ni wanachama wa chama cha ACT Wazalendo kwa tuhuma za kuwakashifu viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa kauli za uchochezi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Viongozi hao walitoa kauli hizo wakiwa katika kikao cha ndani cha chama wakati wakitoa maoni ya kupinga uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idrissa Faina.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Disemba, 2022 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba, Abdalla Hussein Mussa amesema viongozi hao wamekamatwa jana tarehe 10 Disemba, 2022.

Amewataja viongozi hao waliokamatwa kuwa ni Salum Abdalla Herezi maarufu wa Mwalimu Herezi (65) ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uongozi wa Jimbo la Mtambile mkazi wa Mjimbini.

Mwingine ni Nachia Ali Jamali (39), mjumbe wa kamati ya fedha ya Jimbo la Chambani na mkazi wa Wambaa.

Amesema watuhumiwa hao ambao walitenda makosa hayo tarehe 5 Disemba, 2022 baada ya mahojiano hayo wamechiwa huru na uchunguzi unaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!