Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Vigogo Acacia wasomewa mashtaka 39
Habari Mchanganyiko

Vigogo Acacia wasomewa mashtaka 39

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

VIGOGO katika kampuni ya madini ya Acacia, akiwemo aliyekuwa Makamu wa Rais, Deo Mwanyika na Mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, Alex Lugendo leo tarehe 17 Oktoba 2018 wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 39. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwanyika na Lugendo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina na kusomewa mashtaka yanayowakabili ikiwemo ya kughushi na kula njama pamoja na utakatishaji fedha, huku wengine wanne wakitarajiwa kufikishwa kizimbani hivi karibuni.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya makosa hayo katika nyakati tofauti, ambapo katika shtaka la kwanza la kula njama, wanadaiwa kulifanya mwezi Juni na Novemba mwaka 2008 ndani ya nchi na nje ya nchi.

Mwanyika na Lugendo walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Shadrack Kimoro na Jacqline Nyantole.

Kabla ya kupandishwa kizimbani, watuhumiwa hao walikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tangu juzi tarehe 15 Oktoba 2018, ambapo taarifa ya taasisi hiyo ilitaja sababu za kuwakamata kuwa ni pamoja na matumizi mabaya ya ofisi kwenye tasnia ya madini.

Taarifa ya TAKUKURU ilidai kuwa, watuhumiwa hao walishindwa kusimamia nchi kupata mapato kama ilivyotarajiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!