Sunday , 3 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Vigogo 7 TPA kortini tuhuma za uhujumu uchumi, Takukuru yatangaza zawadi nono
Habari Mchanganyiko

Vigogo 7 TPA kortini tuhuma za uhujumu uchumi, Takukuru yatangaza zawadi nono

Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, itawafikisha mahakamani watumishi nane wakiwemo saba wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa makosa ya rushwa, uhujumu uchumi na wizi wa zaidi ya Sh.8 bilioni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 12 Juni 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru.

Watuhumiwa hao ni Deogratius Bellian Lema, aliyekuwa Mhasimu Mwandamizi wa TPA Makao makuu, Marystella Minja, aliyekuwa Afisa Uhasibu TPA Makao makuu, Thomas Akile, aliyekuwa mhasibu wa Kituo cha BANDARI  Mwanza,na Ibrahim Lusato, aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa Kituo cha BANDARI Mwanza.

Wengine ni Wendelin Tibuhwa, aliyekuwa keshia wa Kituo cha Bandari Mwanza, na Leocard Kipengele, Wakili wa Kujitegemea.

Kapwani amesema, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani leo Ijumaa tarehe 12 Juni 2020.

“Kati ya watuhumiwa hao, watuhumiwa 7 walikuwa wa TPA ambao tayari wameshafukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria, mmoja ni wakili wa kujitegemea ambaye pia ni miongoni mwa Wakurugenzi wa Kampuni ya Mnmengele & Associates pamoja na ELA Advocates na hivyo kufanya idadi ya wtaumiwa hao kuwa wanane,” amesema.

Hatua hiyo ya Takukuru  imechukuliwa baada ya kubaini kwamba watuhumiwa hao kwa pamoja walihusika kutenda makosa ya rushwa na uhujumu uchumi, kutokana na kula njama kutenda makosa, kughushi, kuunda genge la uhalifu.

Makosa mengine wanayodaiwa kufanya ni, kuunda genge la uhalifu, kuwasilisha nyaraka za uongo, kuisababishia mamlaka hasara pamoja na utakatishaji fedha haramu.

“Jambo hilo lililopelekea kusababishia upotevu wa fedha kiasi cha zaidi ya Sh. 8 Bilioni, mali ya TPA,” amesema Kapwani.

Doreen amesema, pamoja na kuwafikisha watuhumiwa hao wanane mahakamni, uchunguzi bado utaendelea kwa lengo la kubaini kiasi kingine cha fedha zilizohujumiwa ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuchukua hatua za kisheria watuhumiwa wengine ambao nao wamehusika katika tuhuma hiyo ili nao waweze kuunganishwa.

Amewataja miongoni mwa wanaotafutwa ni; Arnold Tembe, Wakili na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ela Advocates na Mnengere & Associates ya jijini Dar es Salaam na Chrispin Iranque ambaye ni mfanyabiashara wa Dar es Salaam.

“Tunatoa wito kwa yeyote atakayehusika na taarifa za kuwezesha kupatikana kwa watuhumiwa hawa atoe taarifa katika ofisi yoyote ya Takukuru iliyoko karibu naye na zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwao,” amesema Doreen

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Habari Mchanganyiko

TARURA kujenga madaraja 189 kwa teknolojia ya mawe

Spread the loveWakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imejipanga kujenga...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

error: Content is protected !!