May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vifungo vya nje vyaokoa bilioni 1.5

George Simbachawene

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh. 1.5 bilioni kutokana na kutumika adhabu ya vifungo vya nje kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 3 Aprili 2021, na George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, bungeni jijini Dodoma.

“Kutokana na wafungwa hao kutekeleza adhabu zao nje ya magereza, serikali imeweza kuokoa Sh.1.52 bilioni ambazo zingetumika kuwalisha wafungwa hao kama wangeendelea kukaa gerezani – kwa wastani wa Shilingi 2,500 kwa mfungwa kwa siku moja.

Na kwamba, wafungwa hao wamefanya kazi kwenye taasisi za umma ambazo kama zingeajiri vibarua, zingeigharimu serikali jumla ya Sh.1.62 bilioni sawa na wastani wa malipo ya Sh. 4,000 kwa kibarua kwa siku.

“Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeendelea kutekeleza programu ya huduma kwa jamii na huduma za uangalizi. Programu hizi zinalenga kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani, kuokoa fedha za serikali,” amesema.

Simbachawene amesema, program hiyo imeasisi kuwaepusha wafungwa wasio wazoefu kuiga tabia za kihalifu kutoka kwa wafungwa sugu, kuzipatia taasisi za umma nguvu kazi ya wafungwa badala ya kuajiri vibarua.

Amesema, katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021, wizara ilifanya uchunguzi wa kijamii na kuandaa taarifa za uchunguzi 3,097 zilizowasilishwa mahakamani kwa ajili ya kuiwezesha mahakama kutoa uamuzi wa kuwaweka wafungwa kwenye vifungo vya nje.

“Kupitia taarifa hizo, jumla ya wafungwa 2,253 walihukumiwa kutumikia adhabu zao kwenye jamii ambapo wanaume walikuwa 1,792 na wanawake 461.

“Pia, wafungwa 2,365 walimaliza kutumikia vifungo vyao na kurudishwa kwenye jamii kuungana na familia zao,” amesema.

error: Content is protected !!