SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido), Mkoa wa Kigoma limetengeneza sampuli ya vifungashio vya mafuta ya Mawese vitakavyotumiwa na wakulima wa mafuta hayo. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).
Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 8 Septemba 2021 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigai wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Assa Nelson.
Nelson alitaka kujua serikali imefikia hatua gani kurekebisha vifungashio vya mafuta ya Mawese kwa kuwa wananchi wanaumizwa na kunyonywa kupitia vifungashio vinavyotumika sasa.
Kingai akijibu swali hilo amesema, Sido imetengeneza sampuli ya vifungashio vitakavyotumika kufungashia mafuta ya Mawese ambapo imetengeneza vifungashio vya mafuta lita tano, lita 20 na vifungashio hvivo vipo katika mfumo wa ndoo za chuma.
Pia, naibu waziri huyo amesema, vifungashio hivo vipo tayari na kwamba hatua inayofuata ni kuwasilisha sampuli ya vifungashio hivyo kwa Wakala wa Vipimo (WMA) kwa ajili ya uhakiki na mara baada ya uhakiki huo vifungashio hivyo vitawasilishwa Sido ili viweze kuzalishwa kwa wingi kwa ajii ya kufungashia mafuta hayo.
Ametumia fursa hiyo, kutoamaagizo kwa Sido ikishiriakana na WMA kuharakisha uzalishaji wa vifungashio.
Amesema, vizalishwe kwa wingi na endapo kutakuwa na baadhi ya marekebisho kutoka kwa wakala wa vipimo, marekebisho ya vifungashio hivyo yatolewe kwa haraka ili wakulima wa Mawese wasiendelee kunyonywa kama ilivyokuwa mwanzo.
Kutokana na majibu hayo, baadhi ya wabunge wameuliza maswali ikiwemo ni mikakati gani serikali imeweka katika kutekeleza mambo yaliyoombwa na wananchi kufanyiwa kazi na waziri mkuu?
Pia, swali jingine ni je, ni lini vifungashio rasmi vya viazi vitapatikana kwa wakulima wa viazi Makete?
Majibu ya swali la kwanza, Kingai amesema, serikali imezisikia changamoto zote zinazowakabili wakulima wote na inaanza mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto izo kwa wakulima.
Swali la pili ni kwamba serikali imeunda timu maalumu na timu hiyo inapaswa ije na mikakati maalumu ya vifungashio vya mazao maalamu na sio viazi tu ili kuepusha unyonyaji uliopo kwa wakulima.
Asante sana kwa hilo.
Ninaamini vitatufikia na huku Mbeya (Rungwe Na Kyela), na Tabora (Urambo). Hizi sehemu nazo wanalima zao la Michikichi.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Real Estate Investment Consultant