Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Vifo vya wajawazito tishio Moro
Afya

Vifo vya wajawazito tishio Moro

Wajawazito wakiwa hospitalini
Spread the love

VIFO vya wajawazito vimeonekana kuongezeka mkoani Morogoro hadi kufikia vifo 83 mwaka 2016 dhidi ya 68 vilivyotokea mwaka 2015 kutokana na kutokuwepo na mchakato maalum wa kitaalamu wa kujifungua, anaandika Christina Haule.

Kiongozi Mkuu wa mradi wa Huduma Salama za Uzazi (ASDIT), Dk. Angelo Nyamtema amewaambia Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Waganga Wakuu na Waganga wa Vituo vya Afya wakati wa kutambulisha mradi huo.

Dk. Nyamtema amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha vifo hivyo vinakwishwa kwa kutoa mbinu mbadala za kupambana navyo.

Amesema kuwa pamoja na kuongezeka kwa vifo hivyo lakini mradi huo unapambana kuvipunguza pamoja na vifo vya watoto chini ya miaka mitano na ulemavu unaotokana na mchakato wa kujifungua kwa kuangalia viashiria vyake na visababishi ili kuvipatia ufumbuzi wa kudumu.

Naye Mratibu wa mradi huo, Zabron Abel amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo ya vifo kwa wajawazito na watoto wachanga wameamua kuanzisha mradi unaolenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya hususani wa uzazi wa dharura kwa wakina mama kwa lengo la kuwawezesha utoaji wa huduma kwa kiwango cha juu ikiwemo kuwafanyia upasuaji inapobidi.

Aidha amesema kuwa mradi huo utawajengea uwezo watoa huduma za afya ili kuweza kutoa huduma za dhalula katika vituo vya afya ikiwemo kufanya upasuaji kwa kushirikisha watalaam kwa njia ya mawasiliano pale wanapopata kesi za dharula kwa kinamama wajawazito.

Amesema kuwa mradi huo utashirikisha vituo vya afya vitano katika wilaya nne za Morogoro, Kilosa, Mvomero, Gairo ambazo zipo katika mazingira magumu.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Frank Jacob, amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya vifo vinavyotokana na uzazi lakini kupitia mradi huo watalaam wa afya watapewa mbinu mbadala ikiwemo za mafunzo ya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wajawazito ili kuepusha vifo hivyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Stephen Kebwe, almewaagiza watalamu wa afya kuendelea kuboresha huduma ya mama na mtoto ili kunusuru vifo vinavyojitokeza hasa kwa wajawazito na kufanya tafiti mbambali juu ya kushuka na kuongezeka kwa vifo dhidi ya akinamama na watoto.

Dk, Kebwe amesema ipo haja ya watalamu kujikita zaidi katika uboreshaji wa utoaji huduma kwa wajawazito na watoto ili kupunguza vifo vinavyojitokeza na kuendelea kufanya tafiti dhidi ya vifo vya akina mama na watoto.

Ongezeko la vifo hivyo limepelekea Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Afya ya Ifakara kwa kushirikiana na Serikali ya Canada kuamua kwa pamoja kupambana ili kupunguza kasi ya vifo hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!