Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Vifo vilivyotikisa dunia 2022
Makala & UchambuziTangulizi

Vifo vilivyotikisa dunia 2022

Spread the love

WAKATI ikiwa imesalia  siku moja kwa 2022 kufika tamati, dunia haitosahau vifo vya watu mashughuri vilivyotikisa ndani ya mwaka huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, kwa msaada wa mitandao…(endelea).

Mnamo tarehe 8 Septemba mwaka huu, dunia ilitikiswa kufuatia kifo cha kiongozi wa kimila wa muda mrefu wa Uingereza, Malkia Elizabeth II, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 pamoja na kuliongoza taifa hilo kwa miaka 70, kuanzia 1952.

Mtoto wake wa kwanza, Prince Charles alirithi mikoba ya mama yake na sasa ndio Mfalme wa Uingereza. Mwili wa Malkia Elizabeth ulizikwa maeneo ya Windsor jijini London, tarehe 19 Septemba 2022.

Si viongozi wa Bara la Ulaya peke yake, bali wa dunia nzima walituma salamu zao rambirambi kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth, huku mazishi yake yakihudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali , akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, ambao walipata miailiko.

Huku viongozi wa Urusi wakishindwa kuhudhuria baada ya kutopewa mualiko kufuatia hatua yake ya kuivamia kijeshi Ukraine.Nchi nyingine ambazo viongozi wake hawajahudhuria kwa kukosa mualiko ni Belarus na Myanmar.

Shinzo Abe

Kifo cha Malkia Elizabeth II kilitanguliwa na kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe (67), kilichotokea tarehe 8 Julai 2022, hospitalini alikokuwa anapatiwa matibabu ya majeraha ya risasi aliyopigwa alipokuwa anahutubia wananchi katika Mji wa Kusini wa Nara, nchini humo.

Kifo cha Abe kilitikisa dunia kutokana na mazingira ya kiongozi mkubwa wa Taifa la Japan kupigwa risasi hadharani, lakini pia kutokana na wadhifa mkubwa alioushika enzi za uhai nchini humo kwa muda mrefu, kati ya 2006 hadi 2007 na 2012 hadi 2020, alipojiuzulu kwa sababu za kiafya.

Wakati 2022 ukibakisha takribani siku mbili kumalizika, ulimwengu wa soka duniani ulikumbwa na huzuni kufuatia kifo cha nguli wa soka raia wa Brazil, Edson Arantes do Nascimento, maarufu kama Pele, aliyefariki dunia tarehe 29 Desemba mwaka huu kwa matatizo ya figo na kibofu.

Pele aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, alijizolea mashabiki wa soka duniani kufuatia kipaji chake cha kucheza mpira alichojaaliwa na Mungu, ambapo anasifika kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia kwenye mechi 1,363 ndani ya miaka 21.

Pia, Pele anasifika kwa kuwa mchezaji pekee aliyeshinda kombe la dunia mara tatu, 1958, 1962 na 1970. Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo Ijumaa hadi Jumapili, ili kuenzi mchango wake katika soka la nchi hiyo. Mwili wake umepangwa kuzikwa Santos nchini Brazil, baada ya kuagwa kwenye Uwanja wa Vila Belmiro.

Kiongozi mwingine wa kimataifa aliyefariki dunia ndani ya mwaka huu ni aliyekuwa Rais wa China kuanzia 1993 hadi 2003, Jiang Zemin (96). Alifariki dunia tarehe 30 Novemba 2022 kwa matatizo ya saratani ya damu.

Jose Eduardo dos Santos


Kifo kingine kilichogonga vichwa habari ulimwenguni kilikuwa cha Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, kilichotokea tarehe 8 Julai 2022 akipatiwa matibabu kwenye hospitali moja nchini Uhispania, akiwa na umri wa miaka 79.

Kifo cha dos Santos hakikuteka vichwa vya habari kutokana na wadhifa wake , lakini pia suala hilo lilitokana na utata wake, kufuatia familia yake kudai kwamba aliuawa kwa kupewa sumu, kitendo kilichopelekea mahakama nchini Uhispania kutoa amri ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi, hata hivyo matokeo yake yalidai kwamba hakuwekewa sumu.

Kifo cha dos Santos aliyeiongoza Angola kwa takribani miaka 40, kiliibua gumzo zaidi baada ya familia yake kugoma mwili wake kufanyiwa mazishi ya kiserikali, ikidai kwamba alitelekezwa akiwa hospitalini wakati anapatiwa matibabu.

Mnamo tarehe 22 Aprili 2022, Taifa la Kenya lilimpoteza Rais wao wa zamani, Mwai Kibaki aliyeliongoza katika kipindi cha miaka 10 mfululizo, kuanzia 2002 hadi 2013. Mwili wa Kibaki ulizikwa kijijini kwake Othaya, Nyeri tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Kiongozi mwingine aliyefariki dunia 2022 ni aliyekuwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan, aliyeuaga ulimwengu huu tarehe 13 Mei 2022, akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!