July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vifaa vya uchaguzi vyakamilika Dodoma

Spread the love

MSIMAMIZI wa uchaguzi, wilaya ya Dodoma Mjini, Augustino Kalinga amesema maandalizi ya vifaa vya uchaguzi katika jimbo hilo limekamilika na hakuna tatizo lolote. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kukamilika kwa vifaa hivyo amesema kuna ulinzi wa kutosha kwa kila kituo kwani vifaa vyote vinasambaza kila kituo kwa uangalizi na usimamizi mkubwa wa askari kwenye siraha.

Alitoa uhakika wa kukamilika kwa vifaa hivyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa gazeti hili juu ya maandalizi ya kuwepo kwa vifaa hivyo.

“Hapa kwetu vifaa vyote vimekamilika na yapo magari ya kutosho ya kusambaza vifaa hivyo kila kituo na kila kituo kina usimamizi wa askari mwenye silaha.

“Tumefanya hivyo kwa ajili ya kuhakikisha kila kituo kinafunguliwa kwa muda ambao umepangwa yaani saa moja kamili na hilo ili kazi ya kupiga kura ifanyike bila kuwa na kisingizio chochote,” amesema kalinga.

“Hadi sasa sisi hatuna changamoto yoyote ambayo tumekutana nayo kwani vifaa vyote vinatosha, yapo magari ya kutosha wapo askari wa kutosha na hapa kwetu kama unavyoona hakuna mvua hivyo tuna uhakikia na usambazaji wa vifaa na vitafika katika vituo vya kupigia kura vikiwa salama,” amesema.

MwanaHALISI Online ilishuhudia magari zaidi ya saba yakiwa yanapakia vifaa kwa ajili ya kuvisambaza kila kituo huku askari wenye silaha pamoja na mgambo wakiwa katika ofisi za halmashauri.

error: Content is protected !!