December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Video ya ngono ya Waziri yavuja, aomba radhi

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba yuko katika wakati mgumu baada ya video ya ngono iliyomhusisha yeye na mkewe kuvuja mitandaoni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika utetezi wake kupitia akaunti yake ya Twitter, jana aliandika kuwa, video hiyo imevujishwa na wahalifu wa mtandaoni walio ingilia simu yake, huku akidai kwamba ni miongoni mwa mashambulizi ya kisiasa yaliyoanza kuibuka tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Fedha Machi 31, 2017.

Gigaba amejitetea kuwa, alijirekodi video hiyo kwa ajili ya matumizi yake binafsi lakini imesambazwa na wahalifu baada ya mawasiliano yake kuingiliwa.

“Mke wangu na mimi tumejifunza, tumejutia na kuhuzunika kuona kwamba video ya ngono ambayo ilikuwa kwa ajili ya macho yetu imeibiwa wakati mawasiliano yangu yameingiliwa. Nachukua fursa hii kuomba msamaha kwa umma na familia yangu hasa watoto wangu, mama yangu, mkwe wangu kwa maumivu na aibu kufuatia video hii iliyosambazwa mitandaoni,” aliandika Gigaba Twitter.

error: Content is protected !!