VIDEO iliyowekwa na Chuo cha Darul Uloom Haqqania, Pakistan kwenye mitandao ya kijamii ikiwasifu wanamgambo wa Taleban, imeitia hasira Serikali ya Pakistan. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).
Kwenye video iliyowekwa Desemba 2020, iliwaonesha viongozi wa Darul Uloom Haqqania wakijigamba kuwaunga mkono Taliban huku ikiikasirisha Serikali ya Kabul ambayo inapambana kukomesha vurugu mjini humo.
Serikali ya Kabul imeongeza juhudi kukabiliana na vurugu wakati huu, ambapo Marekani ipo kwenye maandalizi ya kuondoa jeshi lake nchini humo.
Kwenye video hiyo, Maulana Yousaf Shah ambaye ni kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa katika chuo hicho, alionesha tabasamu wakati akipitia orodha ya wahitimu wa chuo kikuu hicho.
Wahitimu wengi kwenye chuo hicho walikuja kuwa viongozi katika harakati ya Taliban.
Ameeleza kuwa, amefurahishwa na ushindi wao dhidi ya mataifa yenye nguvu duniani katika vita nchini Afghanistan.
Darul Uloom Haqqnia imetengeneza vigogo wa nafasi za juu wa Taliban.
Wengi wao wakiorodheshwa katika makundi maalumu ya mazungumzo na serikali ya Kabul ya kukomesha vita vilivyodumu kwa miaka 20 sasa.
“Urusi ilisambaratishwa na wanafunzi na wahitimu wa Seminari ya Darul Uloom Haqqania na Marekani pia kufungishwa virago,” alizungumza Shah.
Wakosoaji wameipa jina la Chuo Kikuu cha Jihad.
“Tunajivunia kuimarika kwa kampasi ya Akora Khattak nchini Pakistani, iliyopo karibu kilomita 60 sawa na maili 35 Mashariki mwa Peshawar.
“Sasa inawahudumia wanafunzi takribani 4,000 ambao hulishwa, huvishwa na kusomeshwa bure,” amesema.
Ikampasi hiyo imewekwa njia panda katika ghasia za mapambano ya kijeshi ya kikanda kwa miaka kadhaa.
Imekuwa ikiwaelimisha wakimbizi wa Pakistan na Afghanistan, ambao miongoni mwao wamerudi nchini kwao na kuanzisha vita dhidi ya Warusi na Wamarekani.
“Seminari kama Haqqania huzalisha watu wenye fikra za jihadi, huandaa Taliban na hutishia ustawi wa nchi yetu,” alisema Sediq Sediqqi ambaye ni Msemaji wa Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani, kupitia Shirika la Habari la AFP.
Aidha, viongozi wa Afghanistan wanadai kuwa uamuzi wa Pakistan kuzitambua madrassa hizo ni ushahidi tosha kuwa, wanaunga mkono harakati za Taliban Shah alidhihaki dhana ya kuwa madrassa huhimiza vurugu, wakati huohuo akitetea haki ya kushambulia majeshi ya kigeni.
“Ikiwa mtu mwenye silaha ataingia nyumbani kwako na kuwa tishio kwa Maisha yako… bila shaka utainua bunduki,” alisema Shah.
Mwanzilishi wa Taliban aliyekuwa kiongozi wa seminari hiyo Sami-Ul-Haq, anaijigamba kwa kushauri kuwa mwanzilishi wa harakati ya Taliban, Mullah Omar kuwa anastahiki kuwa kiongozi mkuu yaani ‘baba wa Harakati ya Taliban.’
Baadaye Haq aliwatuma wanafunzi kwenda katika harakati za mapambano, hii ilikuwa baada ya wito wa vita kipindi ambacho Taliban ilikuwa ikipigania madaraka miaka ya 1990.
Mtandao wa Haqq, Kundi la Taliban lenye vurugu kali lilipewa jina hilo kutokana na shule (madrasa) ambayo kiongozi wake mkuu alikuwa akifundisha na ambapo viongozi wengine walisomea.
Baadhi ya Wapakistan wenye msimamo mkali ambao baadaye waliishambulia nchi yao, nao wamehusishwa na seminari hiyo.
Miongoni mwa wahitimu was chuo hucho, ni pamoja na aliyejitoa muhanga na kumuua aliyekuwa Waziri Mkuu was nchi hiyo, Benazir Bhutto.
“Chuo cha Haqq kimejiweka katikati ya mitandao muhimu na yenye ushawishi mkubwa katika madhehebu ya Sunni” alisema mchambuzi Michael Semple.
Inafikiriwa kuwa idadi kubwa ya wahitimu wa vyuo nchini Afghanistan, watakubali nyadhifa na majukumu katika miundo ya makundi ya Taliban.
Hata hivyo, Semple alitupilia mbali dhana yakuwa madrasa zilikuwa “kiwanda cha magaidi” ambapo wanafunzi walipata mafunzo ya kijeshi au walishiriki katika maamuzi ya kimkakati ya vikundi vya wapiganaji.
Badala yake, kama ilivyo kwa wasomi wa vyuo vikuu vya nchi za Magharibi, wamejazwa talanta mpya ndani ya vyama vya siasa, mchango wa harakati za Haqq katika uasi umeghushiwa katika mafunzo yake.
Wahitimu walisisitiza kuwa, hawakupewa mafunzo ya kijeshi na wala haikuwa shuruti kujiunga na vuguvugu za kivita nchini Afghanistan.
Hata hivyo, walikiri kuwa dhana ya jihadi ilijadiliwa wazi ikiwa ni pamoja na katika mihadhara maalumu iliyotolewa na wahadhiri wa Kiafghanistan.
“Mwanafunzi yeyote aliyehitaji kwenda jihadi, aliweza kwenda kipindi cha likizo,” alisema kiongozi wa kidini Sardar Ali Haqqani ambaye ni muhitimu kutoka Seminari hiyo mwaka 2009.
Tatizo kubwa la vyuo hivyo vyenye msimamo mkali, vilipata msaada mkubwa na pesa nyingi miaka ya 1980 wakati vikitumika kama njia ya kueneza jihadi iliyopinga harakati za Kisovieti, vikisaidiwa na Marekani pia Saud Arabia.
Chama cha Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan kilizipongeza vyuo hivyo kwa kuvipatia mamilioni ya Dola za Marekani.
Baadhibya maofisa wa serikali na wanaharakati, wameonya juu ya kuegemea zaidi vyuo hivyo wakidai, wanafunzi wamechanganywa na viongozi wa dini wenye msimamo mkali, ambao hutoa tunzo kwa wanafunzi wanaokaririshwa Quran dhidi ya masomo ya msingi kama vile Hesabati na Sayansi.
Hata jeshi la Pakistan ambalo limekuwa likishutumiwa kuunga mkono harakati za Taliban, limekiri kuwa vyuo vya namna hivyo (vyuo vya kidini) zimezidisha hali ya mashaka katika ukanda huo.
Mwaka 2017, kamanda wa Jeshi la Pakistan, Javed Bajwa aliuliza juu ya wanafunzi takribani milioni 2,500,000 waliokuwa wamejisajili katika vyuo vya namna hiyo.
“Je! Watakuwa viongozi wa kidini au watakuwa magaidi?
“Wamarekani watakapoondoka Afghanistan, tutakuwa katika wakati mgumu sana, kwa kuwa huo ni ushindi kwao,” alisema Pervez Hoodboy, mwanaharakati anayepinga makundi yenye misimamo mikali nchini Pakistan na kuongeza:
“Ushindi wao utawafanya kuwa na ujasiri.”
Leave a comment