Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Vicoba Temeke yaiomba Serikali ‘kuipiga jeki’ viwanda vidogo
Habari Mchanganyiko

Vicoba Temeke yaiomba Serikali ‘kuipiga jeki’ viwanda vidogo

Baadhi ya wanachama wa Vicoba Temeka
Spread the love

TAASISI ya Vicoba endelevu Temeke imeiomba serikali kuiunga mkono katika jitihada zake za kuanzisha viwanda vidogo, ili kufikia uchumi wa kati kwa wanachama wake na taifa kwa ujumla. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na wanachama wa taasisi hiyo katika uzinduzi wa jina la Taasisi ya Vicoba Endelevu Temeke, ambalo ni ‘Temeke Pamoja’, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mratibu wa Taasisi ya Vicoba endelevu Temeke, Johari Mkonde aliitaka serikali kuwapa eneo kwa ajili ya kuanzisha mashine ya kusaga ikiwa ni miongoni mwa miradi iliyopangwa kutekelezwa na taasisi hiyo.

“Tunaiomba serikali itusaidie kupata eneo, tupo tayari kuchangia gharama kama kutakuwa na uhitaji. Taasisi yetu ina dhamira ya kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda. Kwa sasa tunahimiza wanachama kujiwekea hisa na kukopa ili kuendeleza miradi mbali mbali ambayo baadhi tumeanza kuitekeleza,” alisema Mkonde.

Mkonde alisema kuwa, tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, idadi ya vikundi imeongezeka kutoka vikundi 20 kwa mwaka jana hadi kufikia 152 mwaka 2018, na kwamba wana malengo ya kuongeza vikundi na wanachama ili kuongeza idadi ya wanufaika wa Vicoba kupitia ujasiriamali na miradi inayotekelezwa na taasi hiyo.

Naye Rais wa Taasisi ya Vicoba Endelevu nchini, Devotha Likokola aliwataka wanachama wa Temeke Pamoja kujikita katika uanzishaji wa miradi mipya ikiwemo viwanda vidogo ili kufanikisha azma ya taifa ya kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda vidogo.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva alipongeza jitihada za taasisi hiyo, na kuwahimiza wanachama wake kutumia huduma za kibenki pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha ili wafike mbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!