December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vichwa vya treni vilivyotelekezwa TPA vyapata mwenyewe

Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Tanzania, Profesa Makame Mbarawa amemaliza utata uliodumu kwa zaidi ya miaka mitatu juu ya vichwa 11 vya treni vilivyoingizwa nchini humo kuwa vilikuwa vya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Vichwa vya treni vya treni, vilivyotengenezwa nchini Afrika Kusini, vilipokelewa Bandari ya Dar es Salaam, tarehe 21 Machi 2015.

Aliyeibua uwepo wa vichwa hivyo ni aliyekuwa Rais wa Tanania, Hayati John Pombe Magufuli Julai 2017 wakati akizindua mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam akisema kuna vichwa vya treni vilishushwa katika bandari hiyo lakini mmiliki wake hajulikani na kuongeza huo ni mchezo mchafu.

Siku hiyo ya uzinduzi, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko vichwa hivyo vina nembo ya TRC huku akidokeza kwamba kulitokea kutokuelewana baina ya TRC na mtengenezaji wa vichwa.

Leo Ijumaa, tarehe 12 Novemba 2021, Profesa Mbarawa akizungumzia miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara jijini Dodoma, waandishi wa habari alimuuliza nini kinaendelea juu ya vichwa hivyo vya treni na kama kuna waliohusika hatua zimechukuliwa.

Akijibu swali hilo, Profesa Mbarawa amesema, “ni kweli vilikuja na tilipokuwa tunauliza vya nani kila mmoja anavikataa.”

“Ni TRC waliviagiza ila mkataba ulikuwa haijakamilika ndiyo maana walikuwa wanavikataa. Kwa sasa vinatumika na vinaleta faida kubwa sana,” amesema Profesa Mbarawa

Aidha, Profesa Mbalawa amesema, bado kunauzembe kwa baadhi ya wakandarasi ambao wanashindwa kufanya kazi kwa viwango vinavyokubalika.

Hata hivyo, katika taarifa yake, waziri huyo hakutaka kuzungumzia masula ya madei yanayolikabili Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kusababisha baadhi ya ndege kukamatwa nchi za nje.

Amesema suala hilo ni zito na yeye anayo miezi mitatu tu katika wizara na kudai yaliyopita yamepita na shirika liko salama na ndege zipo salama.

error: Content is protected !!