September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vichanga vyafariki baada mama zao kumeza viagra

Spread the love

WATOTO wachanga takribani 11 wamefariki dunia nchini Uholanzi kutokana na mama zao kupewa dawa ya kuongeza nguvu za kiume inayofahamika kama Viagra. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kina mama hao wakati wa ujauzito walifanyiwa utafiti kwa kupewa dawa ya Viagra ili kuimarisha ukuwaji wa watoto ambao hawajazaliwa kutokana na kuwa na kondo la nyuma lisiloimarika.

Kufuatia athari hiyo, Uholanzi imesitisha utafiti huo mara moja baada ya kubainika kwamba Viagra iliyotumika kwa ajili ya kuimarisha usambazaji wa damu katika mwili huenda iliharibu afya ya watoto hao hasa sehemu ya mapafu.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya afya wametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kamili ili kubaini ukweli wa sakata hilo.

Chanzo: BBC Swahili

error: Content is protected !!