August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viboko washambulia mazao Morogoro

Spread the love

WAKULIMA wa Kijiji cha Ihohanja, Malinyi mkoani Morogoro wanaweza kufikwa na njaa kutokana na wanyama aina ya viboko kushambulia mahindi yao shambani, anaandika Christina Haule.

Mpepo Bonavencha Kiwanga, Diwani wa Kata ya Kilosa ameeleza kuwa, wanyama hao wamekuwa tishio kutokana na kushambulia mahindi katika mashamba ya wakazi wa Msanganyego, Ihohanja.

Kiwanga amesema kuwa, wakulima hao wameamua kulima mahindi katika msimu huu kutokana na zao la mpunga kuharibiwa na mafuriko msimu wa masika uliopita.

Kiwanga ametoa wito kwa Mamlaka ya Wanyama Pori kuhakikisha wanadhibiti wanyama hao kwa faida ya hifadhi lakini pia faida ya wananchi katika kulinda mazao yao.

error: Content is protected !!