KANISA la Bikira Maria la Orthodox, lililopo Ngecha, Kiambu Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi limelalamika kuibiwa kengele yake ya shaba yenye kilo 500. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).
Kanisa hilo limeeleza kuomba watu kusaidia kutafuta kengele hiyo, na kwamba tayari taarifa ya upotevu huo imefikishwa polisi na katika vyombo vya habari nchini humo.
Mbali na kengele hiyo, kanisa hilo limelalamika kupoteza limepoteza chupa 10 za mvinyo, vifaa vya matangazo ya nje na vitu vingine hata kabla ya kuibiwa kwa kengele.
Hata hivyo, waumini wa kanisa hilo wamelalamika hatua ya serikali kuzuia mikusanyiko ya dini na kwamba, imesababisha wizi kuongezeka makanisani.
Kenya ni miongoni mwa nchi duniani zilizozuia mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na maeneo ya ibada kama hata za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19).
Leave a comment