October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Veta kujengwa kila halmashauri Tanzania

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendeleza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (Veta) kwa kila halmashauri. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Hayo yamesemwa jana Ijumaa, tarehe 17 septemba 2021 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Tanzania, wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Veta, wilayani Buhingwe, Mkoa wa Kigoma.

Majaliwa alisema chuo hicho kitagharimu Sh.2.4 billion mpaka kukamilika kwake na mpaka sasa chuo hicho kimetumia kiasi cha Sh.1 6 bilion mpaka hapo kilipofikia.

Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Dk. Pancras Bujulu alisema “ujenzi wa chuo hicho gharama zote ni za serikali hivyo kinatarajiwa kuanza kutoa mafunzo ifikapo Januari 2022. Mpaka sasa majengo 15 kati ya 17 yameshaezekwa.”

Aidha, Majaliwa ameipongeza Veta kwa kusimamia na kufuata maagizo ya serikali ya kuanza ujenzi wa chuo hicho kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknolojia “endeleeni kuwa na imani na serikali yenu’.’

Waziri mkuu huyo alisema “tulianza na ujenzi wa vyuo vya Veta kimoja kimoja kila Mkoa, sasa tunashuka chini kwenye kila halmashauri.”

Pia, Majaliwa aliendelea kutoa msisistizo wa utekelezaji wa agizo la Rais Samia juu ya ujenzi wa vyuo vya Veta nchini Tanzania akiwa anaweka jiwe la msingi katika chuo cha veta Buhingwe kwa kusema kuwa

“Chuo hichi nimeweka jiwe la msingi leo kwa maana yake hakitasimama, kitajengwa mpaka kikamilike kwa ajili ya vijana wetu kupata eneo la kujiongezea ujuzi,” amesema.

Majaliwa alisema ujenzi wa vyuo vya Veta katika kila halmashauri ni kuhakikisha vyuo hivyo vinatoa ujuzi maalamu kwa ajili ya vijana wa kitanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo utaalamu wa Tehama, ufundi umeme, ufundi makenika na meneo mengine muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Awali, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kapanga alisema katika awamu ya kwanza wanajenga vyuo vya veta 29 na zitatumika zaidi ya Sh. 48.6 billion kwa ajili ya ujenzi.

Kapanga alisema, ”tutasimamia ujenzi wa vyuo hivi kwa weledi na umakini ili kuhakikisha maono ya Rais Samia yanatimia.”

error: Content is protected !!