July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Van Gal ‘out’, Mourinho ‘in’ Man Utd

Spread the love

KLABU ya Manchester United imetangaza kuachana na Kocha wake, Luis van Gaal, huku nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na Jose Mourinho muda wowote kuanzia sasa, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Pamoja na Van Gaal kuipa ubingwa wa Kombe la FA, lakini klabu ya Manchester United imethibitisha kuachana na Mholanzi huyo kutokana na kutotimiza malengo ya klabu hiyo.

Van Gaal aliyejiunga na Manchester msimu uliopita, alipewa malengo ya kuhakikisha timu hiyo inashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kwa kushinda nafasi nne za juu, kitu ambacho ameshindwa kufanya hivyo.

Mourinho ndiye anayetarajiwa kutangazwa muda wowote baada ya kutupiwa virago Van Gaal, na taarifa zinaeleza kuwa yupo njiani kutua katika jiji la Manchester kumalizana na klabu hiyo.

error: Content is protected !!