Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Uzalishaji mashuleni waokoa wanafunzi
Elimu

Uzalishaji mashuleni waokoa wanafunzi

Wanafunzi wakiendeleza kampeni ya kupanda miti
Spread the love

MRADI wa kuhamasisha shule za msingi kushiriki katika shughuli za utunzaji wa mazingira na uzalishaji mali shuleni, “eco school” umefanikiwa kuongeza mahudhurio ya wanafunzi darasani katika shule ya msingi Kigugu iliyopo kata ya Sungaji, Mvomero, anaandika Christina Haule.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Gaudence Anthony amesema hayo wakati akizungumza na wageni walioanzisha mradi huo mashuleni walipotembelea shule hiyo.

Alisema, awali mahudhurio ya wanafunzi shuleni yalikuwa siyo mazuri na kwamba walikuwa wanafika kati ya wanafunzi 25-30 darasani huku baada ya mradi huo kuanza mahudhurio yameanza kurejea na kufikia wanafunzi 43-48 katika darasa lenye wanafunzi 50.

“Mradi una faida nyingi kwa wanafunzi kwa sababu unapunguza utoro kwa wanafunzi na kuinua taaluma kwa wanafunzi pia mradi unasaidia jamii,” amesema Anthony

Aidha amesema mradi huo umeweza kuendeleza ushirikiano kwa kugawa mbegu za viazi lishe ili wananchi wakapande majumbani mwao lakini pia watoto wao wanauwezo wa kutoa elimu hiyo majumbani na kwamba mradi huo umesaidia sana katika wilaya hiyo.

Naye Ofisa Elimu vifaa wilaya ya Mvomero, Paul Gailanga amesema kwa sasa kamati ipo katika hatua ya ufuatilia katika shule za msingi zilizoingia katika mradi wa eco school, ili kuangalia kilichofanyika tangu mradi kuanza hadi sasa wakati mradi unaingia katika awamu ya pili.

Aidha Gailanga aliwataka viongozi wa shule zilizokashika mradi huo kuona umuhimu wa kufanya uchunguzi wa mazingira ya kuzunguka shule zao ili kuona changamoto zilizopo ili kuzisaidia shule hizo kupitia mpango wa eco schools.

Naye mwenyekiti wa kamati ya eco school, Idd Mbwana ambaye pia ni mmoja wa mzazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Kigugu amekiri ufaulu kuongezeka shuleni hapo na kwamba wanafunzi wenyewe wamekuwa na mwamko mkubwa wanapotoka nyumba wanakuwa na shibe pia wakirudi wanakuta chakula kimeandaliwa ukitofautisha na zamani mwanafunzi akirudi nyumbani huku na njaa hakuti chakula.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Rehema Ally wakieleza jinsi ambavyo wanavyonufaika na mradi huo: “Yaani tumepata faida kubwa sana tumejifunza mambo mengi kupitia mradi huu, tumejifunza kutengeneza tambi, ambazo tunauza na kupata hela ambazo zinasaidia kukarabati wa majengo yetu ya shule, pia tumejifunza kutengeneza unga wa uji wa viazi.”

Naye Sadi Mwakalonge amesema kuwa aliweza kuitumia vyema elimu hiyo kwa kuwafundisha na marafiki zake ambapo ametoa ushauri kwa walimu wa shule mbalimbali hapa nchini wafike shuleni kwao kujifunza.

Mradi wa eco school ambao upo chini ya shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG, unafadhiliwa na Serikali ya Denmark ambayo ni muungano wa nchi nne ambazo ni Tanazania, Malawi, Uganda na Denmark, kwa awamu ya kwanza ya mradi umefanyakazi katika shule za msingi 20, wilayani Mvomero na unatarajia kuongeza idadi ya shule katika awamu ya pili ya mradi kutokana na kuonekana kufanya vizuri katika awamu ya kwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!