December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

UWT wamwangukia Rais Samia

Katibu Mkuu wa UWT, Dk. Phillis Nyimbi

Spread the love

 

UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), umemuomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, atatue changamoto zinazoukabili, ikiwemo ukosefu wa mitaji ya kuendeleza miradi yake na uchakavu wa vifaa vya usafiri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Jumamosi, tarehe 23 Oktoba 2021 na Katibu Mkuu wa UWT, Dk. Phillis Nyimbi, katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya umoja huo, yaliyofanyika wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

“Pamoja na mafanikio mazuri na shughuli tunazofanya, tukiendelea kuwa jumuiya ndani ya CCM, jumuiya yetu inakabiliwa na changamoto angalau hizi naomba nitumie fusra hii kuzieleza. Tuna uhaba au upunfufu wa mitaji wa kuweza kuendeleza miradi mikubwa,” amesema Dk. Nyimbi.

Dk. Nyimbi amesema “ tuna maono mazuri ndani ya jumuiya tunakwama kwenye suala la mitaji, lakini tunaendelea kupanua wigo vyanzo vyetu vya mapato. Tukusanye tuelete chachu ya mapinduzi ya kiuchumi ndani ya jumuiya yetu.”

Kuhusu changamoto ya uchakavu wa vifaa vya usafiri, Dk. Nyimbi amesema inakwamisha shughuli za jumuiya hiyo kwa kuwa vinahitaji marekebisho ya mara kwa mara.

“Tunao upungufu wa vitendea kazi, vyombo vya usafiri tunavyoitumia ni vya muda mrefu vinatumia marekebisho makubwa, ukiachilia kwamba vimechoka. Hii ni changamoto yetu na muda mwingine inapelekea kwenye speed kuchelewa kidogo,” amesema Dk. Nyimbi.

error: Content is protected !!