January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Uvinza ni shamba la serikali’

Waziri wa Kilimo na Chakula, Godfrey Zambi

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa, Shamba la Uvinza ni mali yake Na.206 lenye ukubwa wa hekta 15,000 na sio jambo la vijiji. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kilimo na Chakula, Godfrey Zambi, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Amesema kuwa shamba hilo lilikuwa ranchi ya mifugo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Amesema, mwaka 1994, eneo hilo lilitolewa ili litumike kwa wakimbizi wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Zambi ameongeza kuwa, baada ya wakimbizi kurudi kwao, mkoa wa Kigoma uliiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi  ili shamba hilo litumike kwa shughuli za maendeleo kama vile kujenga makao makuu ya wilaya ya Uvinza na uwekezaki katika kilimo na mifugo kwa barua yenye Kumb Na.CD131/133/01 ya 27 Februari 2010.

Aidha, Zambi amesema 2011, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ilikubali kutoa shamba hilo kwa mkoa wa Kigoma yenye Kumb. Na BA252/433/01 ya 2 Februari mwaka 2011, kwa ajili ya malengo yaliyohainishwa ikiwemo suala la uwekezaji katika kilimo na mifugo.

Mbali na hilo, amesema kuwa, Septemba 2011, shamba hilo lilipimwa na kutengenezewa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Kwamba, baada ya Kampuni ya AgriSol kuwasilisha TIC maombi ya kuendeleza shamba hekta 10,000 mwaka 2012, TIC iliipa kampuni hiyo mkataba wa upangishaji kwa ajili ya uwekezaji kwa mujibu wa sheria ya ardhi Na.6.

error: Content is protected !!