May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UVCCM yampa tuzo Rais Samia, mambo 3 yatakwa

Spread the love

 

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amemtaja mambo matatu turufu kwa Rais Samia Suluhu Hassan yanayomfanya kung’ara kwenye uongozi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mambo hayo ni upangaji, usimamiaji na utekelezaji.

Shaka aliyasema hayo jana Jumapili, tarehe 16 Januari 2022, jijini Dar es Salaam wakati akipokea tuzo ya kumpongeza Rais Samia kwa utendaji mzuri, iliyotolewa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Shaka alimtaja Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM ni mwanadiplomasia nguli wa uchumi na hilo linadhihirika kwa namna alivyopata mkopo nafuu kutoka Shirika na Fedha la Kimatafa (IMF) wa Sh.1.3 trilioni na namna alivyopanga matumizi yake.

Alisema Rais Samia amekuwa turufu ya maendeleo ya Watanzania kutokana na falsafa tatu anazozitumia katika uongozi wake ambazo ni upangaji, utekelezaji na usimamiaji.

Kwa mujibu wa Shaka, hayo yamejidhihirisha katika uongozi wake kwa kipindi cha miezi tisa tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais John Magufuli.

Shaka alisema katika kipindi hicho umeshuhudiwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025, kwamba wanaamini kufikia mwaka 2025 utekelezaji utazidi asilimia 100.

“Kwa kipindi hiki kifupi cha uongozi wake, leo hii ukimsimamisha Mkuu wa Wilaya yoyote akueleze mafanikio, atatumia zaidi ya saa nane kueleza kazi kubwa imefanywa kwa muda mchache,” alisema

Shaka alisema Rais Samia amekuwa kiongozi ambaye kila anachokikusanya anahakikisha kinakwenda katika shughuli lengwa, jambo linalothibitisha usimamizi mzuri.

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM

Pamoja na mambo mengine, alibainisha tuzo hiyo waliyomiabidhi Rais Samia ni ishara ya vijana kuiunga mkono wa serikali ya awamu ya sita.

Aliwataka vijana kuwa mabalozi wazuri wa Rais Samia kwa kueleza mazuri anayofanya, akiwasihi wasipofanya hivyo hakuna mtu wa nje ya nchi atatekeleza hilo badala yao.

“Mcheza kwao hutunzwa basi nanyi vijana hakikisheni mnakuwa mabalozi wazuri wa Rais wetu, ni sisi ndiyo wa kumtia moyo hakuna mwingine atakayefanya hivyo badala yetu,” alisema.

Aliahidi kuandaa darasa la itikadi kwa ajili ya kuwaelimisha vijana, wafahamu nchi ilipotoka, ilipo sasa na inapoelekea.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la UDSM, Isack Sambuli, alisema tuzo hiyo waliyotoa kwa Rais Samia imetokana na utendaji mzuri aliouonyesha kwa kipindi kifupi.

Aliahidi kumtetea na kumuunga mkono wakati wote, akisema vijana hawatarudi nyuma katika hilo.

error: Content is protected !!