Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa UVCCM yaanza kusukwa upya
Habari za SiasaTangulizi

UVCCM yaanza kusukwa upya

Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kusuka upya uongozi wa umoja wake wa vijana (UVCCM). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ni baada ya waliokuwa viongozi wake, nafasi ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu mkuu kuteuliwa kwenye nafasi kadhaa za uongozi ikiwemo, ukuu wa wilaya.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 22 Juni 2021 na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka, akitoa maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dodoma, chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Shaka amesema, kamati hiyo ya imemteua Kenani Kihongosi, kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, ambaye atakwenda kuratibumchakato wa kujaza nafasi za viongozi wa umoja huo zilizoachwa wazi.

“Kihongosi ameteuliwa na Kamati Kuu ya CCM, kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na uteuzi wa juzi alipangiwa Iramba.”

“Lakini kabla ya hapo ameshika nafasi mbalimbali ndani ya CCM, ikiwemo Mwenyekiti UVCCM Iringa, akawa mkimbiza mwenge kitaifa,” amesema Shaka.

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka

Kihongosi alikuwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019. Pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Iringa, hadi Juni 2020, alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli, kuwa Mkuu wa Wilaya Arusha.

Shaka amesema, Kihongosi anachukua mikona ya Raymond Mangwala, aliyeteuliwa na Rais Samia, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, hivi karibuni.

Mbali na uteuzi huo, Shaka amesema nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM iko wazi, baada ya aliyekuwa anaishikilia, Kherry James, kuteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.

Pia, nafasi ya Makamu Mwenyekiti UVCCM iliyokuwa ikishikiliwa na Tabia Mwita, iko wazi baada ya mwanasiasa huyo kuteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, kuwa Mwakilishi na kisha Waziri wa Vijana visiwani humo.

Kenani Kihongosi Katibu Mkuu (UVCCM)

Mwenezi huyo wa CCM amesema, nafasi hizo zimeachwa wazi kwa kuwa katiba ya chama hicho hairuhusu mtu mmoja kushika nyadhifa mbili.

“Kwa kanuni yetu ya uchaguzi wa CCM, hawa kwa uteuzi huu ambao wameupata, wameondoka katika nafasi zao. Kusema kwamba nafasi zote ziko wazi, nafasi ya mwenyekiti na makamu iko wazi,” amesema Shaka.

Shaka amesema, nafasi hizo zitajazwa baadae “kwa hiyo nafasi hizo zitajazwa kwa utaratibu ambao chama kitaelekeza hapo baadae.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!