August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UVCCM wajitosa ujenzi wa vyoo

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis

Spread the love

UMOJA wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Kongwa wametangaza kujitolea kujenga matundu mawili ya choo cha walimu katika shule ya sekondari ya Iduo, anaandika Dany Tibason.

Vijana hao wameanza zoezi hilo jana ikiwa ni moja ya mikakati yao ya kuinua maendeleo katika wilaya hiyo kufuatia hali mbaya ya ukosefu wa choo cha walimu shuleni hapo, hali iliyowalazimu walimu kutumia choo kimoja na wanafunzi.

Asia Halamga, katibu UVCCM, Kongwa amesema, “vijana wa CCM tumeguswa na changamoto ya shule hiyo na zoezi hilo halitaishia hapo tu bali tutazunguka wilaya nzima,” amesema.

Eliasi Mafita, mwalimu wa afya shule ya sekondari Iduo, amemshukuru hatua ya vijana hao kujitolea kujenga vyoo hivyo kwani walimu walipata shida kutumia choo kimoja na wanafunzi.

“Ilikuwa ngumu sana kutumia choo na wanafunzi wakati mwingine unaweza kuwa chooni mwanafunzi akaingia, unakosa hata uhuru wa faragha  na inaleta picha mbaya kiukweli ndugu mwandishi,” amesema Mafita.

Valentino Seng’unda, diwani wa kata ya Iduo, aliwapongeza vijana hao kwa uamuzi wa kufanya shughuli za maendeleo katika wilaya yao na kuwaomba kutoishia hapo kwani changamoto ni nyingi mno.

error: Content is protected !!