January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UVCCM Mwanza wamkana Mtemi

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis

Spread the love

SIKU moja baada ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mwanza, Mtemi Yaledi, kuwataka wananchi kupuuza agizo la Mkuu wa Mkoa huo, Magesa Mulongo, vijana wa baraza hilo wameibuka na kudai kutomtambua. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, amesema katika umoja wa baraza la vijana Mkoa huo hawamtambui Yaledi na wala hawajamtuma.

Amesema katika agizo la Mkuu huyo wa Mkoa alilotolewa Julai 6 Mwaka huu, halikuwa na maana ya kuwakataza wananchi wa Mwanza kwenda Dodoma bali ilikuwa ni kuzuia baadhi ya watu ambao wanadaiwa kuandaliwa kwenda kufanya vurugu wakati wa kupitishwa jina la mgombea wa CCM Julai 13.

“Huyo Yaledi anazuia agizo la RC ambaye ni mwakilishi wa Rais yeye kama nani, ni mtu mmoja ambaye anaongoza genge moja la kihuni la 4u Movement ambalo linatumika na watu wachache kutaka kuhatarisha hali ya usalama.

“Kwenye Katiba ya CCM hatuna chombo hicho cha kihuni na hukuna sehemu yeyote kiliposajiliwa ndani ya chama chetu, kama umoja wa vijana Mkoa tunakanusha kuwa na mjumbe anaeitwa Mtemi Yaledi, tumeshangaa kuona kauli yake ya kupingana na Serikali,” amesema Kimu.

Kimu amesema watanzania wanapaswa kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanya Oktoba Mwaka huu kwa baadhi ya watu wanaotumia Mwanya wa vijana kufanikisha adhma yao ya maisha.

Amesema Serikali inapaswa kuwa makini na baadhi ya watu wanaosafiri kwenda Dodoma, kwani wengi wao wanatumiwa wagombea wa nafasi ya Urais kwa ajili ya kwenda kufanya vurugu endapo majina yao yatakatwa.

 

error: Content is protected !!