April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Uvamizi Segerea’: Mdee, Bulaya waanza kusota Kisutu

Spread the love

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe na wenzake 14, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya vurugu katika gereza la Segerea. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).   

Kwenye kundi hilo, wapo wajumbe wanne wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na wanachama 10 wa chama hicho.

Bmali na Mdee, wengine ni Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Jesca Kishoa, Mbunge Viti Maalumu; Boniface Jacob, Meya wa Ubungo na Henry Kilewo, mjumbe wa kamati hiyo, wamefikishwa mahakamani hapo leo tarehe 23 Machi 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema katika ukurasa wake wa Twitter, watuhumiwa hao walitakiwa kuripoti polisi leo, lakini wamepelekwa mahakamani.

Mdee na wenzake wanatuhumiwa kufanya fujo katika Gereza la Segerea, walipokwenda kumtoa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, aliyekuwa anatumikia kifungo cha miezi mitano gerezani hapo.

Kwa mujibu wa Chadema, hadi sasa watuhumiwa hao hawajapandishwa kizimbani.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE kwa taarifa zaidi…

error: Content is protected !!