January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uturuki kuwajengea kituo Albino

Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Spread the love

UBALOZI wa Uturuki nchini Tanzania, umeahidi kujenga kituo maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Anaandika Sarafina Lidwino… (endelea).

Kituo hicho kitakuwa na huduma zote za kijamii, kama vile hospitali, shule na ulizi mkali utawekwa maeneo hayo.

Bernard Membe- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa- ndiye ametoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa mazunguzo baina yake na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.

Membe amesema, kila ifikapo mwisho wa mwezi ,mabalozi hao hukutana na kuzungumzia masuala mbalimbali duniani, yakiwemo machafuko yanayotokea Tanzania na kuangalia jinsi ya kuyatatua.

Amesema katika kikao hicho pia amewagusia kuhusu mashambulizi yaliyotokea kule Tanga kwenye mapango ya Amboni na mauaji ya Albino yanavyoendelea nchini.

Kwa mujibu wa Membe, suala la mauaji ya Albino, Serikali imeshaaza kuchukua hatua kwa watuhumia 15 ambao walitiwa hatiani na mahakama wamehukumiwa kunyongwa  hadi kufa ili kuyakomesha.

“Serikali ina mpango wa kukomesha ukatili huu unaofanywa na baadhi ya watu waliokosa elimu, wakidhani Albino ni chanzo cha mafanikio yao. Tutahakikisha mauaji haya yanabaki kua ziro,” amesema Membe.

error: Content is protected !!