Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Utumbuaji sasa wapiga hodi kwa vikosi vya SMZ
Habari za Siasa

Utumbuaji sasa wapiga hodi kwa vikosi vya SMZ

Spread the love

MAOFISA kadhaa wa ngazi ya juu, kutoka vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi za umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Miongoni mwa waliosimamishwa kazi, ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa bohari kuu ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), makao makuu Kibweni, Unguja; msaidizi mkuu wa Bohari hiyo na msaidizi wake mkuu namba mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Ijumaa, tarehe 15 Januari 2021, mjini Unguja, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za (SMZ), Masoud Ali Mohammed, ameeleza kuwa serikali imechukua hatua hiyo, ili katika mkakati wake wa kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Alisema, “tumechukua maamuzi haya kwa sababu rushwa, ni mbaya na ubadhilifu wa mali ya umma, ni mbaya. Lakini pia hatuwezi kukaa kimya kwa kuwa wenzetu wamefanya juhudi za kufanya uchunguzi na kutoa taarifa.”

Ameongeza, “…kwamba watuhumiwa wote hawa, wanahusika katika makosa ya kuhujumu uchumi, ubadhilifu, wizi wa mali ya umma na udanganyifu.”

Amesema, serikali imeamua kuchukua hatua hiyo, ili kuuhakikishia umma kuwa masuala ya wizi na ubadhilifu wa mali ya umma, hayakubariki na rais na hayakubariki na utawala wa awamu ya nane Visiwani.

Waziri Mohammed, amewataja maofisa wengine alioamuru wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi, ni Naibu Kamishena Mkuu wa kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU), ambaye kwa sasa, ndiye Kaimu Kamishena Mkuu wa kikosi hicho, Gora Haji Gora.

Wengine waliosimamishwa kazi, mkuu wa utawala wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), na amemuagiza atakayekaimu nafasi ya mkuu wa utawala na fedha wa kikosi cha Zimamoto, kumsimamisha kazi, mkuu wa utumishi wa Kikosi cha Zimamoto ili kupisha uchunguzi.

Aidha, waziri huyo amesema, kwa mamlaka aliyonayo amemuagiza atakayeteuliwa kukaimu nafasi ya mkuu wa utawala na fedha kwa kikosi cha Zimamoto, kumsimamisha kazi mhasibu wa kikosi hicho.

Waziri Mohammed amemuagiza Kamishena mkuu wa Chuo cha Mafunzo, kumsimamisha kazi, mara moja, mhasibu mkuu wa chuo cha Mafunzo (MF).

Uchunguzi uliomsukuma serikali kuchukua maamuzi ya kuwasimamisha kazi vigogo hao wa ngazi ya juu kwenye vikosi hivyo, umefanywa na mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Visiwani – Zanzibar Anti-Corruption and Economic Crimes Authority (ZAECA).

Akizungumza huku akionekana kukerwa na vitendo hivyo, waziri Mohammed amesema, mbali na kusimamishwa kazi viongozi hao, ameagiza kusimamishwa kazi maofisa wengine waliotajwa kwenye tuhuma hizo.

Amesema, taarifa aliyoitumia kuwasimamisha kazi wahusika, imefafanua kwa kina, uhusika wa kila mmoja na imeeleza tuhuma moja baada ya nyingine.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!