Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko UTPC yataja mchango wa Rais Samia katika sekta ya habari
Habari Mchanganyiko

UTPC yataja mchango wa Rais Samia katika sekta ya habari

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa rafiki wa wanahabari, kufuatia dhamira yake aliyoionesha tangu alipoingia madarakani Machi 2021, ya kuifanyia maboresho sekta ya habari, hususan katika sheria zake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 14 Desemba 2022 na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC), Deogratius Nsokolo, akizungumzia mwenendo wa mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia sekta ya habari nchini.

“Rais Samia tangu alipoungia madarakani, alikuwa karibu na sekta ya habari na kutoa matumaini ya kufanyiwa marejeo kwa sheria hi ya mwaka 2016. Na tayari matokeo yake ni wadau wa habari na serikali kukaa kwa pamoja na kuainisha vipengele gani tungependa viondolewe,” amesema Nsokolo.

Rais huyo wa UTPC, amesema dhamira njema ya Rais Samia kwa sekta ya habari imezidi kujidhihirisha kufuatia agizo lake la Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, kukutana na wadau wake, ili kujadili namna ya kuondoa vikwazo dhidi ya uhuru wa habari, ikiwa pamoja na kuondoa sheria kandamizi.

“Upande wa serikali na wadau umeishamaliza kazi yake ya kuainisha vipengele hivyo, kilichotarajiwa ni mwaka huu mwezi wa tisa mapendekezo hayo kupelekwa bungeni lakini kwa bahati mbaya haikuwezekana.

“Serikali kwa uwazi kabisa ilieleza sehemu mkwamo kwamba, Waziri (Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) alisema, mapendekezo hayo hayakufikishwa bungeni kwa kuwa kuna hatua zilikuwa hazijakamilika. Hii ni dhamira ya wazi kabisa ya serikali hii,” amesema Nsokolo.

Amesema, kazi iliyobaki sasa ni upande wa Serikali kukamilisha mchakato na kisha mapendekezo hayo kupelekwa bungeni kwa mujibu wa sheria za nchini.

“Wito wangu, mchakato huo uende kwa kasi ile ile kwa sababu mabadiliko hayo yatawezesha waandishi wa habari kuwa huru zaidi, pia kufanya kazi zao kwa weledi kwa sababu, vile vitu ambavyo tuliviona ni vikwazo, vitakuwa vimeondolewa,” amesema Nsokolo na kuongeza:

“Mambo hayo yanayokwaza uhuru wa habari yakiondolewa, yatasaidia sana maendeleo ya nchi yetu kwa sababu, habari ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.”

Naye  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema mchakato wa marekebisho ya sheria unakwenda kwa kasi kwa sababu Rais aliyepo madarakani ana dhamira njema na sekta ya habari.

Na kwamba, baada ya wadau wa habari kufanya vikao serikali, wadau wanasubiri matunda ya vikao hivyo kwa kupelekwa mapendekezo ya wadau wa habari bungeni.

“Katika mchakato huu, tumekuwa tukishiriki kuzungumza na waziri husika ili tukubaliane katika sehemu mbalimbali ya vifungu vya sheria ya habari.Tulifanya mkutano wa mwisho mwezi Novemba ambao tulisema, sasa huu uwe mkutano wa mwisho ili sheria ya huduma za habari ipelekwe bungeni,” amesema Balile.

Hivi karibuni, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa alisema serikali inajiandaa kuwasilisha bungeni mabadiliko ya vipengele vya Sheria ya Huduma za Habari ili wabunge wakiridhia utekelezaji wake ufanyike.

“Kwa sasa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inajiandaa kuwasilisha bungeni mabadiliko ya sheria hii ili wabunge wakiridhia, tuendelee na utekelezaji wake,” alisema Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!