October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Utovu wa nidhamu wamuondoa Mkude kambini Stars

Jonas Mkude

Spread the love

 

KIUNGO wa klabu ya Simba Jonas Mkude ameondolewa kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu mara baada ya kuchelewa kuripoti kambini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Stars imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar 2022, dhidi ya Benin utakaochezwa Oktoba 7, 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya kambi hiyo zimeeleza kuwa wachezaji hao walitakiwa kuripoti kambini siku ya Jumapili Oktoba 3, 2021 na mwisho wa kuwasili kwenye kambi hiyo ilikuwa ni majira ya saa 11 jioni.

Mtoa taarifa alisema kuwa Mkude akiwa moja ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi hiko alitoa taarifa ya kuchelewa kuripoti kambini kwenye muda uliopamngwa was aa 11 jioni, na hivyo uongozi ulikubali ombi lake na kumtaka mpaka kufikia saa tatu awe tayari ameshafika.

“Mkude aliomba ruksa ya kuchelewa kuingia kambini na uongozi ukakubali ombi lake na kumtaka mpaka kufikia saa tatu usiku awe ameshafika, lakini cha kushangaza Mkude alifika kwenye kambi hiyo majira ya saa 5 usiku jambo ambalo halikuwafurahisha wengi na kumtaka akaendelee na shughuli zake,” kilisema chanzo hicho.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa nje ya kikosi cha Taifa Stars kwa muda mrefu mara baada ya kusimamishwa na uongozi wa klabu yake ya Simba Desemba 28, 2020 kufuatia kuwa na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Stars akiwa hajacheza mchezo hata mmoja wa kimashindano ndani ya klabu yake ya Simba toka Desemba 2020.

error: Content is protected !!