April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Utouh alianzisha, aungana na Prof. Assad

Ludovick Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu

Spread the love

LUDOVICK Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, ameungana na Prof. Mussa Assad, CAG wa sasa kwamba, Bunge linashindwa kusimamia serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Utouh ametoa kauli hiyo ikiwa ni zaidi ya miezi sita kupita tangu malumbano kati ya Prof. Assad na Job Ndugai, Spika wa Bunge yaibuke baada ya Prof. Assad kusema kuwa, Bunge ni dhaifu.

Prof. Assad alitoa kauli hiyo kwenye mahojiano na mwandishi wa kituo cha redio cha Umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Kauli hiyo, ilionekana kumkera Spika Ndugai na hata kumwita Prof. Assad kujieleza na kuomba radhi mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge jambo ambalo, Prof. Assad aliendelea na msimamo wake ‘dhaifu’.

Utouh alizungumzia mvutano kati ya Spika Ndugai na Prof. Assad wakati  wa uwasilishaji wa uchambuzi wa ripoti za CAG kwa miaka mitatu, jijini Dar es Salaam.

Kwenye uwasilishaji huo Utouh alihoji sababu za mawaziri kumshambulia Prof. Assad na kuonya kwamba, kazi ya Prof. Assad sio ya kisiasa na hawakuwa na nafasi hiyo.

“Zile kazi za CAG sio siasa, waziri anapanguaje ripoti ya CAG?” alisema Utouh ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwajibikaji wa Umma (Wajibu) na kuongeza kwamba, ripoti ya Prof. Assad inaeleza nani anahusika wapi.

Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani alimvaa Prof. Assad kwa kudai kuwa ni muongo na kwamba, yupo tayari kuongozana na mdhibiti huyo kuonesha sare za Jeshi la Polisi kwamba zipo kwenye makontena.

Lugola alitoa kauli hiyo baada ya ripoti ya Prof. Assad kueleza kuwa, licha ya Sh. 16 Bilioni kutumika kwa ajili ya ununuzi wa sare hizo, hakuna ushahidi kwamba, sare hizo zililetwa.

error: Content is protected !!