Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Utetezi wa Mbowe neno kwa neno Kisutu
Habari za Siasa

Utetezi wa Mbowe neno kwa neno Kisutu

Spread the love

NOVEMBA 4, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema alianza kutoa ushahidi wake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kwenye kesi hiyo ya uchochezi namba 112/2018, washtakiwa ni Mbowe, Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu – Zanzibar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Akiongozwa na Kibatala, Mbowe alisema:-

Kibatala: Umesema majina yako ni?

Mbowe: Freeman Aikael Mbowe

Kibatala: Unaishi wapi?

Mbowe: Mikocheni, Dar es Salaam

Kibatala: Mikocheni ipi?

Mbowe: Mikocheni ‘A’

Kibatala: Unafanya shughuli gani?

Mbowe: Mimi ni mbunge wa jimbo la Hai, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kibatala: Umeanza kuwa mbunge wa jimbo la Hai tangu lini?

Mbowe: Nimekuwa mbunge tangu mwaka 2000.

Kibatala: Unasema nini kuhusu uzoefu katika shughuli za siasa?

Mbowe: Nimeshiriki chaguzi zote kubwa na ndogo ambazo chama chetu zimeshiriki tangu mwaka 1995.

Kibatala:  Umesema kuwa umeshiriki chaguzi zote tangu mwaka 1995 na umekuwa mbunge mwaka 2000 huku nyuma uligombea nafasi gani?

Mbowe: Nimesema nimekuwa Mbunge mwaka 200 lakini nimeanza tangu 1995.

Kibatala: Nafasi nyengine ulizogombea?

Mbowe: Niligombea Urais mwaka 2005 kupitia Chadema.

Kibatala: Vitaje vyama vingine viwili vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo?

Mbowe: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mgombea wake Jakaya Kikwete na Chama cha Wananchi (CUF), mgombea alikuwa Profesa Ibrahim Lipumba.

Kibatala: Ulishika nafasi ya ngapi kwenye uchaguzi huo?

Mbowe: Nafasi ya tatu.

Kibatala: Hilo jina la Freeman limetokana na nini?

Mbowe: Ni jina ambalo wazazi wangu wameamua kunipa kwani nilizaliwa wakati wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, na nilipatizwa siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba mwaka 1961 kwa maana hiyo, wazazi wangu wakanipa maana ya jina la Freeman maana yake ‘mtu huru’.

Kibatala: Kwa kifupi wazazi wako wana historia gani kwenye hii nchi?

Mbowe: Wazazi wangu ni wanasiasa walipigania Uhuru na kipekee baba yangu ndiye Mwasisi wa Tanu Kanda ya Kaskazini. Mama yangu alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Tanu, Mkoa wa Kilimanjaro muda mrefu tangu 1970.

Kibatala: Umekuwa mwenyekiti Chadema kwa muda gani?

Mbowe: Tangu mwezi Septemba 2004.

Inaendelea…..

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!