Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Utekwaji, uteswaji umevuruga Uchaguzi wa Madiwani
Habari za SiasaTangulizi

Utekwaji, uteswaji umevuruga Uchaguzi wa Madiwani

Spread the love

UCHAGUZI mdogo wa kata 43 nchini uliofanyika Novemba 23 mwaka huu umeingia dosari kutokana kuripotiwa kwa matukio ya kupigwa, kutekwa pamoja matumizi mabaya ya nguvu ya dola,  yamevuruga uchaguzi huo, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadmu (LHRC), Anna Henga ameeleza namna uchaguzi huo ulivyogubikwa na vurugu zilizosababisha hofu kwa wapiga kura.

Ameeleza kuwa uchaguzi huo ulifanyika Novemba 26 mwaka huu umepelekea uvunjifu wa haki za binaadamu, matumizi mabaya nguvu yaliyofanywa na nguvu za dola pamoja na watu kutekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kukamatwa na kujeruhiwa kwa lengo kuvuruga uchaguzi na kuwatia hofu kwa wapiga kura.

Mkurugenzi huyo amesema mbali na matukio hayo lakini pia wametekwa kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi CUF, Visiwani Zanzibar.

Amesema wengine wametekwa kata ya Kitwilu Iringa Mjini na kikosi cha ulinzi cha CCM kinachojulikana kama ‘Green Guard’ waliowavamia wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Eliza Nyenzanandugu, Martha Francis wameripotiwa kutekwa wakati wanaenda kupiga kura, kisha kunyang’anywa simu na kuwatelekeza katika msitu wa Kilolo hadi walipopata msaada wa wapita njia,” ameeleza Henga.

Amesema kuwa matukio hayo yameambatana pamoja na kushambuliwa kwa gari la Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Daddy Igogo, huku Jeshi la Polisi likimkamata na kumshikilia Meya wa Manispaa hiyo, Alex Kimbe.

Henga amedai kuwa Kituo hicho kilifuatilia kwa ukaribu matukio hayo na kubaini kuwa vitendo hivi vimeripotiwa kufanywa na vyombo vya dola, watu wasiojulikana na watu wanaosadikika kuwa wafuasi wa vyama vya siasa ikiwemo CCM na Chadema pamoja na vyama vingine vya upindanzani.

Tukio lingine ni kupigwa na kujeruhiwa kwa mawakala na wanachama wa Vyama vya siasa. Imeripotiwa kuwa Mfuasi wa (CCM) katika jimbo la kawe, alivamiwa na kujeruhiwa na watu wanaosadikika ni wafuasi wa chama cha (CHADEMA), hatimaye kulazwa katika Hospitali ya Rabinisia, Tegeta jijini Dar es Salaam. Kama inavyoonekana katika picha hapo chini .
“Katika Kata ya Makiba, wakala wa Rashid Jumanne na Mwenyekiti wa Tawi la Valeska, (CHADEMA) Nickson Mbise wamejeruhiwa kwa kushambuliwa kwa mapangawalipokuwa wakielekea katika vituo vya kupigia kura.”

Henga ameeleza kuwa iliripotiwa kuwa, katibu wa CCM Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu akiwa amelazwa hospitalini baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikika kuwa ni wafuasi wa CHADEMA wakati akiwasindikiza mawakala wa Chama chake kwenda vituoni kwa ajili ya kusimamia upigaji wa kura.

Amesema kuwa vitendo hivyo vimeripotiwa katika kata ya Nyabubhinza, Maswa na Simiyu, Mawakala katika vituo nane(8) kati ya vituo 13 walikamatwa na Jeshi la Polisi ikiwemo Diwani wa CHADEMA Zakayo Chacha Wangwe. Pia, katika kata ya Kimweri wilayani Meatu Emmanuel Nawadi akiwa na mawakala wawili wakielekea kwenye vituo vyao majira ya alfajiri, walivamiwa na kushambuliwa na vijana wanaosadikika wanachama wa (CCM) ambapo diwani huyo alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga.

“Kuna matukio yameripotiwa kuhusu Viongozi wa vyama vya siasa na mawakala wa vyama kukamatwa mathalani Katibu wa (CHADEMA) Wilaya ya Ubungo ambaye alikuwa mratibu mkuu wa uchaguzi wa Kata ya Saranga, Perfect Mwasiwelwa, alikamatwa na Jeshi la Polisi tangu siku ya Tarehe 25. Novemba Mwaka huu pia jeshi hilo lilimkamata Meya wa Ubungo Boniface Jacob aliyekuwa wakala mkuu wa kwenye majumuisho ya kura za mwisho katika Kata.

Henga amesema kuwa Katika tukio lingine, imeripotiwa kwamba Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Sofi, wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro. Rico Venance alikamatwa akiwa anatembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura ambapo ni haki yake kwa mujibu wa taratibu zinazosimamia uchaguzi. Jeshi la polisi halijasema hadi sasa sababu za msingi za kuwakamata na kuwashikilia mawakala na Viongozi hawa wa kisiasa.

Tukio jengine ambalo halijawahi kutokea katika historia ya chaguzi nchini ni kuondolewa kwa mawakala wote wa CHADEMA katika Vituo takribani 13, Kata ya Mamba, Wilaya ya Bumbuli na Tanga, wakati uchaguzi ukiendelea kufanyika na kupelekwa Polisi bila kutajwa sababu ya kukama Waliondolewa katika vituo vyao majira ya saa nne asubuhi siku ya Uchaguzi na kupelekwa kituo cha Polisi na hakuna sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwao. Lakini vile vile Kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA katika Kata ya Ibighi, wilaya ya Rungwe na Jeshi la Polisi bila sababu yoyote kukamatwa kwao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!