Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Utekaji watikisa, hofu yapanda
Habari za Siasa

Utekaji watikisa, hofu yapanda

Spread the love

MATUKIO ya utekaji, utesaji na hata kupotezwa yamekuwa yakitikisa nchi kwa sasa huku wananchi wakipiga yowe, yakomeshwe. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Hali hiyo imewaibua wazee wa Chama cha ACT- Wazalendo, wakiitaka serikali kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kukomesha matukio hayo.

Wilson Mushumbusi, mwenyekiti wa wazee wa chama hicho akizungumza na wanahabari leo tarehe 7 Julai 2019, katika ofisi za chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam amesema, kuna kila sababu kwa serikali kuhakikisha matukio hayo yanakoma.

Mzee huyo amekemea hayo huku zikiwa zimepita siku tatu baada ya kupatikana kwa Raphael Ongangi, mfanyabiashara wa Kenya na msaidi wa Zitto Kabwe ambaye aliokotwa Mombasa, Kenya jirani na kwa shangazi yake.

Ongangi alitekwa akiwa na mkewe Dar es Salaam ambapo alikaa kwenye mikono ya watekaji, watesaji kwa zaidi ya siku tano na hatimaye kupatikana Kenya.

Tukio la Ongangi ni sehemu ya matukio ya utekaji yanayotikisa kwa sasa nchini, huku serikali ikieleza kuwa ‘watu wasiojulikana’ bado hajawapatikana.

Mbele ya wanahabari Mzee Mushumbuzi amesema kuwa, vitendo hivyo viovu vinaharibu taswira ya nchini na kuongeza hofu kwa Watanzania.

Amehoji kwamba, inawezekanaje mtu akatekwa mchana na kisha akaa siku nyingi bila serikali kujua, na hata baadaye akasafirishwa nje ya nchi?

“Wakati mwingine watekaji wanakuwa na silaha, halafu wanateka mchana tena hata mbele za watu,?” amehoji Mzee Mshumbusi akisema kuwa, serikali inapaswa kukomesha vitendo hivyo.

Wakati huo huo Mushumbusi ameitaka Serikali iweke usawa kwa vyama vya siasa ili kupatikane haki na kuimarisha Demokrasia.

Amesema ili haki ipatikane kwenye uchaguzi lazima kuundwe  Tume huru isiyopendelea au kuwa na maslahi kwenye chama chochote    cha siasa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!