May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utatuzi Masheikh wa Uamsho wanukia

Spread the love

 

OTHMAN Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, ameahidi kuendelea juhudi zilizofanywa na mtangulizi wake Hayati Maalim Seif Shariff Hamad na rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi kuhusu masheikh wa Uamsho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Akizungumza katika Msikiti wa Maghfira, Unguja Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021, Othman amesema atashirikiana na Rais Mwinyi katika juhudi hizo.

Masheikh wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi ni Farid Hadi Ahmed, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Anthari Ahmed, Amir Hamis Juma, Abdallah Hassan, Alawi Amir, Mohammed Yusuph, Sheikh Mselem Ali Mselem na Said Sharifu.

Wengine ni Juma Juma, Hassan Suleiman, Salum Ali Salum, Abdallah Said Ali, Hussein Ally, Kassim Nassoro, Abubakar Mngodo, Rashid Nyange, Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Saidi Ally na Salum Amour Salum.

Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Zanzibar

Othman amesema, Maalim Seif wakati wa uhai wake, alishirikiana vizuri na Rais Mwinyi katika kuliangaliajambo hilo, na kwamba ataendelea pale alipoishia mtangulizi wake (Maalim Seif), aliyefariki dunia tarehe 17 Februari 2021.

“Wakati wake (Maalim Seif) alishirikiana vizuri na Rais Mwinyi. Walifanya juhudi kubwa kuhakikisha suala la masheikh wa Uamsho linapatiwa ufumbuzi, juhudi hizo zimefika pazuri. Nitaendelea kuungana na Rais Mwinyi kupatia ufumbuzi suala hilo,” amesema.

error: Content is protected !!