Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Utatu mtakatifu’ wa kupinga rushwa ya barabarani wazinduliwa
Habari Mchanganyiko

‘Utatu mtakatifu’ wa kupinga rushwa ya barabarani wazinduliwa

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau mbalimbali wa kupinga rushwa nchini imezindua kampeni maalum ya kupambana na rushwa barabarani. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo tarehe 1 Novemba, 2019 na kupewa jina la UTATU inatazamiwa kuwa fimbo ya vitendo vya rushwa vinavyofanyika barabarani na wakati mwingine kusababisha kutokea kwa ajali nyingi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kampeni hiyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza ajali za barabarani.

Amesema kuwa inakadiliwa ajali za barabarani katika nchi za Afrika ugharimu zaidi ya asilimia 1 hadi 3 ya pato la taifa kila mwaka na kuwa iwapo kila mmoja atawajibika ipasavyo kupunguza ajali za barabarani inawezekana.

“Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018/19 ajali za barabarani zimeanza kupungua kutokana na juhudi za wadau mbalimbali kupambana na tatizo hilo kwa kushirikiana na jeshi la polisi,” amesema.

Sambamba na uzinduzi wa kampeni hiyo imezinduliwa pia Aplikeshen (App) maalum inayojulikana kama ‘TAKUKURU (PCCB)’ inayowezesha watu kutuma taarifa na matukio ya rushwa kwa njia ya simu popote matukio hayo yanapotokea ili kufikiwa na Takukuru na Jeshi la polisi kwa wakati na kwa haraka ili kuyachukulia hatua za kisheria.

Sabina Seja, Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kutoka Takukuru, amesema kuwa wameamua kuzindua mfumo huo kutokana na malalamiko mengi kutolewa na watu wakiwemo abiria, madereva na hata askari wa usalama barabarani na wakati mwingine ajali za mara kwa mara zikielezwa kuwa chanzo cha rushwa kunakopelekea madereva kuingia na magari mabovu barabarani kwa kutoa hongo wasikamatwe.

“Hii kampeni inaitwa utatu kwa sababu ya ushirikiano wetu na Jeshi la Polisi pamoja na wadau mbalimbali wanaohusika na barabarani, tumefanya hivyo kwa sababu ya umuhimu wa maisha yetu hivyo lengo ni kuzuia ajali za barabarani zinazotokana na vitendo vya rushwa,” amesema Seja.

Amesema kuwa kufanya hivyo kutaondoa sababu za rushwa katika ajali za barabarani, kwa kuwa na magari mabovu, kutifuata sheria kwa sababu tu wameweza kuoenyeza rushwa.

Aidha, IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini amesema kuwa mfumo huo utasaidia kwa sababu inapunguza polisi au vyombo vya ulinzi na usalama kukutana na mtuhumiwa na kuwa suala hilo ni la jamii nzima na ifikie mahala watu waone suala la rushwa Tanzania liishe.

“Utafiti unaonyesha madereva wengi ndiyo wanaoshawishi mapolisi kupokea rushwa baada ya kufanya makosa lakini kuna polisi wachache wanachangia pamoja na wadau wengine,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!