Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Utata wa Sugu uko wapi?
Habari za SiasaTangulizi

Utata wa Sugu uko wapi?

Spread the love

BADO nasisitiza, Sugu ametoka gerezani kwa msamaha wa rais. Lakini nakana kuwa Sugu amesamehewa na rais. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).

Kuna tofauti kubwa sana ya mtu kutoka gerezani kwa msamaha wa rais na rais kumsamehe mfungwa.

Kwa mfano, Babu Seya na familia yake imetolewa gerezani na rais. Hawakutoka kwa msamaha wa rais.

Rais alitamka hadharani kuwa nimesamehe wafungwa kadhaa, akiwamo Babu Seya na familia yake.

Hapa kutoka kwa Babu Seya, hakukuzingatia vigezo vya muda wa kuishi gerezani, adhabu aliyopewa wala kosa alilotenda.

Msamaha ulikuwa mahususi kwake. Maana kama ingekuwa kigezo cha kifungo, Babu Seya alikuwa anatumikia kifungo cha maisha.

Ndani ya magereza wapo wafungwa wengi waliohukumiwa kifungo cha maisha, lakini aliyetolewa kwa msamaha alikuwa Babu Seya na watoto wake.

Kuna waliohukumiwa vifungo vya muda mrefu – miaka 20 hadi 30 – kwa makosa yanayofanana na lile la Babu Seya.

Inawezekana wapo wengine wameishi gerezani muda mrefu zaidi kuliko yeye, lakini bado hawakunufaika na msamaha huo.

Hawakutoka kwa sababu, msamaha wa jumla haukuwahusu na siyo waliosamehewa kwa majina yao na rais.

Hii maana yake nini? Kwamba rais anayo mamlaka ya kikatiba ya kutoa misamaha kwa wafungwa.

Msamaha huo huwa hautaji jina la mfungwa. Unataja masharti ya jumla ya wafungwa wanaopaswa kunufaika.

Hapa rais anakuwa hawafahamu ni akina nani watakaonufaika na msamaha huo.

Anachojua yeye ni kuwa kuna wafungwa watatoka nje kwa msamaha wake.

Orodha ya wanaopaswa kutoka kwa msamaha huo – kutokana na vigezo vya msamaha vilivyowekwa – huandaliwa na magereza.

Kwa mfano, katika suala la Sugu, rais ametoa msamaha wa punguzo ya robo ya vifungo kwa wafungwa takribani 3500.

Wanaopaswa kunufaika ni wale wenye vifungo visivyozidi miaka mitano na wale tayari wametumikia nusu ya vifungo vyao kutokana na ile 2 ya 3 ya muda anaopaswa kuishi gerezani.

Sugu amehukumiwa tarehe 26 Februari kifungo cha miezi mitano. Alipaswa kutoka Agosti bila msamaha wa kisheria wa magereza na tarehe 5 Mei baada ya msamaha.

Kwa maneno mengine, Sugu alipaswa kuishi gerezani siku 100.

Kuafuatia msamaha wa rais, Sugu akapata ahueni ya punguzo ya robo ya kifungo chake. Hivyo akatakiwa kuishi gerezani siku 75.

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni hili: Je, kwa nini Sugu hakutoka siku ambayo rais alitoa msamaha – tarehe 26 Aprili?

Jibu ni kwamba siku hiyo Sugu alikuwa hajamaliza kifungo chake cha siku 75 kilichopatikana baada ya msamaha wa rais na msamaha wa kisheria wa magereza.

Ndio maana ametoka jana tarehe 10 Mei. Hiyo ndio sababu.

Hakuna shaka kuwa wafungwa wengine wataendelea kutoka kadri siku zao zinapomalizika kufuatia msamaha huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!