August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utata juu ya tuzo ya Ronaldo

Cristiano Ronaldo

Spread the love

SIKU chache baada ya mshambuliaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia inayotolewa na moja ya gazeti nchini Ufaransa “Ballon d’Or” kumeibuka na mijadala mingi juu ya mabadiliko ya tuzo hizo kama ni ile inayotolewa na Shirikisho la soka la Dunia (FIFA)

Kwa sasa Ronaldo atakuwa ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya nne nyuma ya mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi ambaye anaoangoza kwa kunyakuwa Ballon d’Or mara nyingi kuliko mchezaji yeyeto katika historia ya tuzo hizo baada ya kushinda mara tano katika miaka tofauti.

Ballon d’Or ilianza kutolewa rasmi mwaka 1956 kwa mchezaji bora wa mwaka kutoka bara la Ulaya, huku kura za kumpata mshindi zikipigwa na waandishi wa habari za michezo kutoka nchini ufaransa kwa kushirikiana na chama cha soka cha nchini humo kama ilivyofanyika kwa mwaka huu.

Mwaka 1995 tuzo hizo ziliendelea kukua na kuhusisha wachezaji wote wanaocheza katika klabu za Ulaya tu na kumfanya George Weah kuwa mwafrika wa kwanza kushinda tuzo hizo kabla ya mwaka 2007 tuzo hizo kuhusisha wachezaji kutoka kila pembe ya Dunia.

Katika kipindi chote hicho cha utoaji wa tuzo hiyo kubwa FIFA wao walikuwa na tuzo yao ya mchezaji bora wa mwaka kabla ya mwaka 2010 rais wa FIFA wa wakati huo, Sepp Blatter alipoamua kuifanya Ballon d’or kuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia inayotolewa na FIFA.

Tuzo hiyo iliyofahamika kama FIFA Ballon d’Or ilianza kutolewa kuanzia mwaka 2010-2015 ambayo mshindi alikuwa anapigiwa kura na wajumbe wanaochaguliwa na FIFA katika mkutano maalumu, huku ikihusisha pia kupata kikosi bora cha dunia kwa mwaka.

Mwaka 2016 raisi wa sasa wa FIFA, Gianni Infantino aliamua Balloon d’Or iendelee kuwa tuzo inayojitegemea kama ilivyokuwa hapo awali, huku FIFA nao wakiwa na tuzo zao za mchezaji bora wa mwaka ambazo zinatarajiwa kutolewa mwezi Januari mwakani.

error: Content is protected !!