December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utafiti wa wafanyakazi wa ndani wapigwa ‘stop’

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, imeipiga marufuku Taasisi ya Haki za Binadamu kufanya utafiti wa unyanyasaji watumishi wa ndani wa kitanzania wanaofanya kazi nchini Omani na Umoja wa Falme za Kiarabu, anaandika Angel Willium.

Ofisa wa Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia, William Kindeketa ambaye ni mwanasayansi amesema watafiti hao hawakufata utaratibu na utafiti umefanyika hapa nchini waliwahoji wafanyakazi walioenda katika nchi hizo.

“Katika nchi yoyote kukitaka kufanya tafiti ni lazima ufate taratibu zinazotakiwa kufuatwa ikiwemo kujaza fomu ya maombi na kupitiwa na watalaamu ili kujua kama imekidhi vigezo,” amesema Kindeketa.

Kwa upande wa Taasisi ya Haki za Binadamu, kupitia kwa Ofisa wake Audrey Kawire amesema leo walitaka kuzindua ripoti ya “kufanya kazi mithili ya roboti,” unyanyasaji wa watumishi wa ndani wa kitanzania nchini Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu, lakini Maofisa wa Costech wamesema tusizindue kwa sababu atukufata utaratibu wakufanya utafiti.

Pia Kawire amesema waliruhusiwa na Wizara ya Mambo ya Nje kutoa ripoti hiyo, hivyo walifuata taratibu zote zinazotakiwa katika utafiti, watu wa Costech wamekuja leo asubuhi walivyotaka kuzindua, wakafanya nao mazungumzo na yalikuwa mazuri, tafiti hii wamefanya wenyewe na wakaandika barua kwa serikali.

Taasisi ya Haki za Binadamu ni ya kimataifa, inayojitegemea ambayo inafanya kazi kama sehemu ya harakati zenye nguvu za kusimamia utu na heshima ya binadamu.

error: Content is protected !!