August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utafiti wa Twaweza wamchambua Magufuli

Spread the love

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Twaweza, imetoa ripoti ya utafiti iliyoufanya kuhusiana na utendaji wa serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli, anaandika Pendo Omary.

Twaweza imetoa matokeo ya utafiti huo leo Dar es Salaam, huku kitendo cha Rais Magufuli kupiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi pamoja na ‘timua timua’ ya watumishi wa umma ikiwa ni miongoni mwa mambo yaliyowakera wananchi.

Utafiti ulifanywa kwa wahojiwa 1,813 kutoka kundi huru la pili la sauti za wananchi, ikiwa ni awamu ya 11 ya simu zilizopigwa kwenye kundi jipya kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni, 206 kwa upande wa Tanzania bara pekee.

“Wananchi walipoulizwa vitendo gani vya Rais Magufuli ambavyo hawakubaliani navyo kabisa, suala la kuzuia uingizaji wa sukari na kupanga bei elekezi. Wananchi watatu kati ya kumi (asilimia 32) walilitaja suala hilo na kusema hawaafikiani nalo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Licha ya wananchi kuunga mkono hatua ya Rais Magufuli kuwaondoa watendaji ambao wanatuhumiwa kufanya vitendo viovu lakini wamepinga utaratibu unaotumika.

“Wananchi nane kati ya kumi ambao ni sawa na asilimia 76 wanasema kuwa watendaji waondolewe pale tu ambapo kuna uthibitisho wa vitendo viovu,” taarifa ya ripoti hiyo imeeleza.

Ripoti hiyo pia imeangazia suala la ufahamu wa wananchi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini, ambapo imeeleza kuwa mwananchi mmoja tu kati ya 20 ndiyo anapata taarifa za kutosha kuhusu masuala ya siasa nchini.

 

error: Content is protected !!