Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko UTAFITI: Vyakula vya baharini, wanyamapori chanzo cha Covid-19
Habari MchanganyikoTangulizi

UTAFITI: Vyakula vya baharini, wanyamapori chanzo cha Covid-19

Spread the love

IMEELEZWA kuwa Soko la vyakula vya baharini na wanyamapori la Huanan lililopo katika mji wa Wuhan nchini China ndio kitovu cha mlipuko wa Virusi vya Ugonjwa wa (Covid-19). Anaandika Faki Sosi Ubwa … (endelea).

Ugonjwa huo ulioibuka Disemba 2019, hadi sasa umeripotiwa kuua zaidi ya watu milioni sita duniani.

Utafiti umefanywa na wanasayansi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Sayansi Marekani (American Association for the Advancement of Science-AAAS) na kuchapishwa tarehe 26 Julai 2022 katika jarida la sayansi la jumuiya hiyo.

Jarida hilo la Sayansi duniani pia limechapisha utafiti mwingine kuhusu chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo ambapo tafiti zote mbili zilizokusanywa kwa namna tofauti zimekuja na matokeo yanayofanana ya kuwa Soko la vyakula vitokanavyo na bahari na Wanyamapori la Huanan huko Wuhan lilikuwa na uwezekano mkubwa wa kitovu cha virusi hivyo.

Utafiti wa kwanza unaonyesha kuwa kesi za kwanza za watu waliobainika kupata virusi hivyo, zilinasibishwa kwa karibu na soko hilo.

“Wakati kesi za mapema za COVID-19 zilizotokea jiji zima la Wuhan, nyingi zilikusanyika katikati mwa mji huo karibu na ukingo wa magharibi mwa Mto Yangtze na msongamano mkubwa wa kesi karibu na soko la Huanan,” utafiti ulinukuu katika jarida la Sayansi.

“Kesi zote nane za Covid-19 zilizogunduliwa kabla ya tarehe 20 Disemba 2019,  zilitoka upande wa magharibi wa soko, ambapo aina ya wanyama waliouzwa walikuwa wanavisaba chanya vya mlipuko wa pili wa virusi hivyo. Tuligundua kuwa kesi za Covid-19 zilienea zaidi katika jengo la soko “utafiti katika jarida la Sayansi unaongeza.

Utafiti mwingine unaotumia maelezo ya kinasaba kufuatilia muda wa mlipuko wa COVID na unapendekeza kwamba kulikuwa na majina mawili ya virusi hivyo.

Utafiti uliochapishwa katika jarida hilo wenye jina la Maambukizi ya molekuli ya asili nyingi za zoonotic ya SARS-CoV-2” na iliyotajwa na chombo cha habari cha CNN inachukua mtazamo wa kimolekula ambapo umebaini lini maambukizi ya kwanza ya virusi hivyo yalitoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Kulingana na utafiti huo, maambukizi ya kwanza kutoka kwa mnyama kwenda kwa mwanadamu yanadhaniwa yalitokea tarehe 18 Novemba 2019  na yalitoka kwa ukoo ‘B’.

Watafiti waligundua zaidi aina ya ukoo ‘B’ katika watu ambao walikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na soko la Huanan.

Matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano kwamba  mlipuko wa pili wa virusi hivyo  ulizunguka kwa wanadamu kabla ya Novemba 2019.

Licha ya kuchukua njia tofauti, tafiti zote mbili zinafikia ushahidi kwamba maambukizi ya pili ya virusi vya Sars-Cov-2 yalikuwepo katika mamalia hai ambao waliuzwa kwenye soko la Huanan mwishoni mwa 2019.

Kulingana na tafiti hizi mbili, virusi vilihama kwa wanyama kwenda kwa wanadamu waliokuwa wakifanya manunuzi kwenye soko hilo.

Tafiti hizi zimekuja mwezi mmoja baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kupendekeza kwamba wanasayansi waendelee kutafiti vyanzo vyote vinavyowezekana vya janga la Covid-19, pamoja na uvujaji wa maabara.

Profesa katika Idara ya Immunology na Microbiology katika Utafiti wa Scripps, Kristian Andersen alisema tafiti hizo hazikanushi nadharia ya uvujaji wa maabara.

“Nilikuwa na hakika kabisa juu ya kuvuja kwa maabara  hadi tulipoingia kwenye hii kwa uangalifu sana na kuiangalia kwa karibu

“Kulingana na data na uchanganuzi ambao nimefanya katika muongo mmoja uliopita kwenye virusi vingine vingi, nimejihakikishia kuwa data inaelekeza kwenye soko hili,” alisema Andersen. Chanzo: zee5. com.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

error: Content is protected !!