January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utafiti REDET ulioota mbawa wavuja

Mtia nia wa CCM, Edward Lowassa

Spread the love

MPANGO  wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET),  inaofanywa na idara ya sayansi ya siasa na utawala ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam ulihahirishwa ghafla umevuja. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Julai mbili mwaka huu vyombo vya habari mbalimbali vilipewa mwaliko  kuhudhuria mkutano huo uliotakiwa kufanyika  Chuo Kikuu julai tano uliota mbawa bila kuwepo na sababu za msingi kwa kile kilielezwa kuwa ni kutokukamilika kwa ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ilivuja kwa wanahabari baada ya Mwenyekiti Mwenza  wa REDET, Dk. Bana Benson  kuwapa taarifa ya kuhairishwa kwa mkutano huo na kuthibitisha kutokamilika kwa ripoti hiyo

Kwa mujibu ya vyombo  vya habari vilivyoiona ripoti hiyo ilikuwa ya kurasa  29 ambayo mbali na suala la urais pia ilimulika maeneo ya utawala, sera na matarajio ya umma katika serikali ijayo.

Ripoti hiyo namba 18 inaonyesha kuwa utafiti huo uliowafikia watu 1,250 kati ya 2,500 waliolengwa katika wilaya 25 mikoa yote huku ikielezwa kuwa watafiti hao hawakuweza kufanya kazi Zanzibar kutokana na kukosa kibali kutoka kwa mamlaka husika.

Urais  kwa upande wa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa aling’ara kwa  kwa kupata asilimia 27  huku Dk. Wilibroad Slaa kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) akipata asilimia 23.1.

Wengine ni  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  Benard Membe (8.2) na kufuatia na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (7.2) 

Urais mbali na Dk. Slaa kupitia (UKAWA) wengine ni Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba (13.6) Mwenyekiti wa chadema Taifa  Freeman Mbowe(7.2) 

Kwa upande wa sifa ya rais ajaye aslimia 36.2 ya wahojiwa wanataka mwadilifu kwa kauli na vitendo, asilimia 24.8 awe na uwezo wa kupiga vita umasikini na unyonge.

REDET inapendekeza kuwa vyama vya siasa vinaweza kutumia ripoti yake kufanya maandalizi mazuri ya ilani za uchaguzi na hatua nyengine za kimataifa kama hatua ya kiviwezesha kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu.

error: Content is protected !!