May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Utabiri wa MwanaHALISI, watimia, Mbunge wa Chadema ang’oka

Spread the love

MBUNGE wa Chadema katika jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro, Dk. Godwin Mollel, amekihama chama hicho. Anaripoti Pendo Omary…(endelea).

Dk. Mollel alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho leo mchana kupitia taarifa kwa umma na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk. Mollel alisema, amechukua uamuzi huo akiwa na akili timamu kwa lengo la kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

 

MwanaHALISI liliandika mwezi mmoja uliopita kuwapo kwa mkakati wa wabunge wawili, mmoja kutoka Chadema na mwingine kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Tayari mbunge wa Kinondoni kupitia CUF ametangaza kujiuzulu.

error: Content is protected !!