KATIKA siku za hivi karibuni, mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Gobless Lema, alijizolea umaarufu wa kutabiria wabunge wenzake, kuondoka chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Kibona Dickson … (endelea).
Mtabiri huyu ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama kinachoendelea kupata maumivu ya kuondokewa na wabunge.
Mtabiri huyu wa twitter alitabiri juu ya Mbunge mmoja wa Kaskazini kuondoka, ikatimia baada ya Dk. Molleli wa Siha kuhamia CCM.
Aliendelea kuandika utabiri na uzushi wake mwingi kupitia twitter zake. Yakitimia, pengine kwa coincidence anazidi kujipatia umaarufu na kuota pembe za kuitwa mtabiri.
Jana, tumesikia “James Ole Millya amejivua uanachama wa Chadema na kujiuzulu ubunge.”
Kulingana na gazeti la Mwananchi la mtandaoni, Lema amesema, “Millya aliishaondoka Chadema siku nyingi na yeye alikuwa anajua.” Lema amekiri kuwa Millya alikuwa rafiki yake.
Ninajiuliza, kwanini mtabiri huyu wa twitter kama alijua siku nyingi, kwa nini hakuandika juu ya kuondoka kwa Millya? Kwanini huyu mjumbe wa kamati kuu hakutoa taarifa hizi kwa chama chake?
Jibu ni moja: Kwamba, James ole Millya ni rafiki yake. Kazi ya Lema si kutabiria marafiki zake, bali kuwazushia, kuwagombanisha na kuwachonganisha, maadui zake ndani ya Chadema.
Niliwahi kuandika kuwa ndani ya Chadema kuna fitina, chuki na mifarakano. Ndani ya Chadema watu hawapendani. Mazingira haya yanachochea watu kukata tamaa; kuwa desperate na baadaye kuangukikia mikononi mwa CCM.
Mabingwa wa fitina chamani pia ni mabingwa wa propaganda. Wanajua kulisha watu propaganda. Kwa kila ahamaye wanataka umma uamini “amenunuliwa” bahati vijana wengi ni walaji na watafunaji wa propaganda.
Kwenye somo la elimu ya viumbe kuna kitu kinaitwa fertilization(yai kurutubishwa). Ili fertilization itokee, panahitajika mbegu ya mwanaume na yai la kike.
Chuki, fitina na faraka ni yai ya kike +mbegu za kiume ni CCM. Kwamba mimba ya wabunge wa Chadema kuondoka inatungwa ndani ya chama kwenyenyewe, katika mazingira ya chuki, fitina na faraka. Watungishaji ni CCM.
CCM wataendelea kumwaga mbegu zao tu…….na wabunge wa Chadema wataendelea kuondoka. Njia pekee ya kuzuia wabunge, madiwani na viongozi wa chama hicho kutoondoka, ni kuangush mnara fitina na chuki ndani ya chama.
Watu aina ya Lema washughulikiwe kwa mujibu wa kanuni za chama.
Dickson Kibona
Mwanaharakati huru..
Spread the love RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...
By Mwandishi WetuMarch 20, 2023Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...
By Mwandishi WetuMarch 16, 2023Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...
By Mwandishi WetuMarch 15, 2023Spread the love KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...
By Mwandishi WetuMarch 14, 2023
Leave a comment