August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Usomaji MwanaHalisi, Mseto warahisishwa

Spread the love

MAGAZETI ya MwanaHALISI na Mseto yanayozalishwa na Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), sasa yanaweza kusomwa popote kwa kutumia ‘application’ ya sim gazeti, anaandika Regina Mkonde.

“Mteja anaweza kusoma kuraa zote bila tatizo. Tumefanya hivyo ili kuongeza urahisi kwa wasomaji wetu lakini pia kuweza kufika mbali zaidi na kwa haraka ikiwa ni ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,” amesema Yusuf Aboud, Meneja Utawala wa HHPL na kuongeza;

“Tulianza na m-paper tangu mwaka jana na sasa tumeungana na sim gazeti kwa lengo lile lile la kufikisha magazeti ya kampuni yetu kwa wateja wetu popote walipo na kwa haraka zaidi.”

Abdillah Muna, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dau Technology LLC iliyoasisi sim gazeti akizungumza na Mwanahalisi Online leo amesema, kusoma gazeti la MwanaHalisi na Mseto kupitia sim gazeti kuna faida nyingi.

“Kwa kutumia sim gazeti bei ya gazeti inakuwa nusu ya ile ya awali kwa maana itakuwa Sh. 500 badala ya Sh. 1000 kama linavyonunuliwa kwenye meza ya magazeti.

“Si magazeti hayo tu, yapo magazeti mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya udaku, dini, michezo na siasa.

“Pia kuna majarida pamoja na vitabu katika sim gazeti ambayo yanauzwa kwa nusu ya gharama halisi,” amesema Muna.

Amesema kuwa, mtu yoyote mwenye simu ya kisasa (smartphone) anaweza kupakuwa (download) kutoka kwenye play store kisha atajisajili na kuanza kupata huduma hiyo.

“Kupitia sim gazeti mtu mwenye mtandao (line) wa Vodacom, Tigo na Airtel anaweza kununua popote alipo na kwa wakati wowote.

“Walio nje ya nchi pia wanaweza kununua MwanaHalisi, Mseto na magazeti pia majarida mengine kupitia huduma ya PayPal. Muda si mrefu tutauunganisha mtandao wa Zantel na huduma yetu ili kufikia wateja wa mtandao huo,” amesema Muna.

 

error: Content is protected !!